Jumanne, 9 Desemba 2014

WAISLAMU WAJITOKEZA KATIKA USAILI WA KUTAFUTA WATANGAZAJI KWENYE KITUO CHA RADIO YA KIKRISTO

Jumamosi iliyopita ulifanyika Kiango Presenters Search, katika hotel ya tamal Mwenge, blog hii ilikuwa pale kufuatilia kila kinachoendelea. washiriki walio jiandikisha walikuwa karibu 30 na kati ya hao wakuwapo waislamu 7 ambao majina yao si vizuri kuyaweka hapa hadhalani na kati ya maswali waliyoulizwa waliulizwa kuwa wanafahamu radio ni ya kikristo na wao walikiri kwa wanafahamu ila wanatamani wapewe nafasi ya kufanya kazi na kiango radio.

Lakini kubwa zaidi pale mshiriki mmoja mkristo alipoamua kumpa Yesumaisha yake aliulizwa swali na chief Dad Fred Msungu kama ameokoka akajibu hajaokoka akaulizwa utaokoka lini akasema hata sasa naweza kuokoka. hiyo ilisisimua sana na aliongozwa sara ya toba na kumpokea Bwana Yesu kati ya washiriki wote waliohudhulia wanatakiwa kupatikana watu wawili ambao majina yatatangazwa muda si murefu.

Kituo cha radio cha Kiango kitaanza matangazo ya live muda si mrefu na kitakuwa kinatangazia kutoka kijitonyama kwani studio ya kisasa imesha kamilika.
Washiriki wakingoja kuitwa ndani

Washiriki wakijiandikisha
Team nzima ya majaji ikiwa kazini

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni