Mwimbaji wa nyimbo
za injili maarufu nchini Tanzania ambaye ni mlemavu wa mkono
mmoja Mwinjilisi Joseph Nyuki maarufu kwa jina la Balozi wa Yesu amejikuta
mikononi mwa polisi wakati akiendesha harambee yake ya Injili mtaa
kwa Mtaa mjini Iringa.
Hapa
ndiyo shughuli ya ukamataji unapoaanza kwa kumtia nguvuni mwimbaji wa
nyimbo za injili mara baada kuanza kuhubiri neno la Mungu kwa njia ya
uimbaji mtaa kwa mtaa.
twende kituoni ukajielezee huko.
mwimbaji Nyuki ambaye anajiita balozi wa Yesu akiwatuliza wafuasi wake.
Mara baada ya kuwatuliza wafuasi wake anakwenda kupanda gari lake kuelekea polisi.
akiwa tayari ndani ya gari lake.
akiondoka mara baada ya kuruhusiwa kuondoka kituoni.
Akizungumza kulezea kulichojiri mara baada ya kuachiwa huru.
Balozi wa Yesu akionyesha CD yake
mpya ya Saluti ambayo alikuwa akiiuza mtaani kabla ya
kuwapigia saluti polisi waliomkamata kwa muda
wananchi wakilizunguka gari la Balozi wa YESU.
Hii ndio CD ya
Saluti ambayo leo balozi wa Yesu kajikuta akiwapigia
kiukweli
Saluti Polisi Iringa.
Tukio hilo la balozi wa
Yesu kukamatwa na polisi limetokea majira ya saa 8
mchana ya tarehe mbili Desemba mwaka huu wakati gari la mwimbaji
huyo wa Injili likipita katika mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa kueneza
injili kwa kuuza CD inayokwenda kwa jina la Saluti .
Mbali na kuwa na
kibali cha Manispaa ya Iringa kinachompa uhuru wa
kueneeza injili kwa watu wote kupitia CD hiyo ya Saluti na
kibali hicho kupitishwa polisi bado askari
polisi walimfuata balozi huyo wa Yesu na kumtia nguvuni kuwa
hapaswi kueneza injili kwa kupiga kelele mitaani.
Askari ambae jina
lake halikuweza kunaswa mara moja alifika katika
gari lenye namba za Usajili T 364 DPD ambalo
lilikuwa limefunga muziki mnene na kupeperusha
injili mtaani kiasi cha kila mmoja mjini hapa kuvutiwa na vionjo
vya mwimbaji huyo na kulifuata gari hilo kununua CD kabla
ya askari huyo kulipiga pini gari hilo eneo
la Soko kuu Miyomboni mjini Iringa .
Baada ya kumsimaisha mwimbaji
huyo kutoendelea na uuzaji wa CD hiyo askari huyo alimtaka
kuonyesha kibali pamoja na kuzima muziki na kugeuza gari hilo kupeleka
Polisi amri ambayo bila jeuri balozi wa Yesu alitii
huku akisema ndio kazi ya kueneza injili hiyo ambayo kwake
ameizoea .
Kwa upande wao
wananchi ambao walikuwa wakinunua CD wameeleza
kusikitishwa na hatua ya polisi kuzuia uenezaji wa injili
huku kila siku mji wa Iringa watu wanapita na magari
wakitangaza Ma Disco na matamasha yenye vichocheo vya maambukizi ya
VVU huku wakiyafumbia macho.
Mtandao huu
ulipofuatilia sakata hilo kituo cha polisi
ulishuhudia suala hilo likiishia nje ya kituo cha
polisi baada ya askari huyo kuyamaliza kiume na mwimbaji huyo
nje ya kituo baada ya kuonyesha kibali halali cha Manispaa ya
Iringa na wakati askari huyo akihoji zaidi juu ya
kuzunguka kila kona likiwemo eneo hilo la polisi kwa
kupiga muziki ghalfa Mungu alionyesha nguvu zake kufuatia
gari jingine lililokuwa likiuza simu huku
likipiga miziki ya duniani likipita nje ya kituo cha polisi
bila kukamatwa ndipo askari kwa kuona hilo walimruhusu
kuendelea na kazi ya kuitangaza injili.
Akielezea tukio hilo
mara baada ya kuachiwa huru Balozi wa Yesu Joseph Nyuki
alisema kuwa polisi walifika na kumsimamisha na
kumwomba kibali na baada ya kuonyesha aliachiwa huru na
kuwa polisi wametimiza wajibu wao na kuwa hana kinyongo
nao.
Pia alisema kuwa
ziara yake mkoani Iringa na mikoa mbali mbali ni kuitangaza
injili kupitia oparesheni yake ya Injili mtaa kwa Mtaa
kwa watu wote waokoke na kuwa anaifanya hivyo
kama njia ya kuuza CD yake baada ya kuchoshwa na
unyonyaji unaofanywa na baadhi ya studio kwa kuwalalia waimbaji wa
nyimbo za Injili nchini.
KWA HISANI http://amaninafuraha.blogspot.com
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 4777775 au Whatup, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni