Jumamosi, 27 Desemba 2014

DVD MPYA YA NIPE NGUVU YA KUSHIDA SASA IKO MADUKANI

Mungu amekuwa mwema kwangu tangia nilipomkubari kuwa mwokozi wangu na nguzo yangu. Nimeona Mungu akinishindia na magumu ninayopitia na niliyoyapitia katika maisha yangu. Nimeona Mungu huyu unayemwabudu kila siku akinivusha na kunitia moyo pale ninapoona akili yangukufikiri jinsi ya kutatua yale yaliyombele yangu. Mungu huyu ni waajabu kwangu, kaniwezesha katika uaandaji wa albamu hii mpya ya "NIPE NGUVU YA KUSHINDA". Nazidi kumshangaa Mungu huruma zake na fadhili zake kwangu.

Flora Mbasha

Ninaamini hata wewe unaweza kufarijika na kuinua imani yako kwa kusikiliza ujumbe ulio ndani ya DVD hii. Mungu wangu anataka kuongea na wewe kwa kupitia uimbaji wangu. Ni maneno ya Mungu ambayo ameweka ndani yangu kwaajili ya kuponya na kuinua imani yako kwa njia ya uimbaji. Kwangu ni vigumu mno kukufikia na kukuhubiria habari njema, lakini kwa kupitia DVD hii utaweza kuungana nami na kupata Neno la Mungu.Hayo ni maneno ya mwimbaji Flora Mbasha.
Flora Mbasha Nipe Nguvu ya Kushinda

Ndugu mpendwa wangu, ninatambua unatamani sana kushinda magumu yaliyoko mbele yako na haya unayopambana nayo, na umekuwa ukijiuliza nitafanya nini? Lakini natamani kukutia moyo na kukuomba uzidi kuwa magoti mwa Mungu wetu kila kuitwapo leo. Acha kusikiliza maneno ya watu wanaokusemea mabaya ila msikilize Mungu wako naye atakutia nguvu.

Nyimbo zilizomo humu zitakusaidia sana katika maisha yako haya. Mungu akubariki sana.

Flora Mbasha Nipe Nguvu ya Kushinda

ANGALIA WIMBO WA NIPE NGUVU YA KUSHINDA

            
 KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni