Jumamosi, 15 Novemba 2014

MWIMBAJI WA INJILI HELLEN CHIWANGA KUTOKA DODOMA YUKO KWENYE MAANDALIZI YA KUTOA ALBAMU YAKE YA PILI CHINI YA JOHN MTANGO

Mwimbaji wa nyimbo za injili Hellen Chiwanga wa Dodoma ambaye alisha wahi kutoa albamu yake kipindi cha nyuma na uzinduzi wake kuwa gumzo katika mji wa Dodoma na viunga vyake kwa kuwajaza vingunge wa bunge la Tanzania katika uziduzi huo cd iliyokwenda kwa jina la NIKULINGANISHE NA NINI. sasa anakuja na albamu yake mpya ambayo inaendelea kurekodiwa chini ya producer nguli wa nyimbo za injili hapa Tanzania tunamzungumzia John Mtango mtoto wa mchngaji aliye muibua Beatrice Mhone katika ile albamu ya ingoje ahadi akiwa na Upendo Kilahiro. soma mwenyewe alivyo andika katika ukrasa wake wa fb.

Dear friends, baada ya kupotea kwa muda mrefu katika tasnia ya uimbaji,nimeamua kurudi na kuanza kumtumikia Mungu wangu kwa njia ya uimbaji..nipo katika hatua za mwisho za kukamilisha audio CD ambayo itafuatia na DVD,soon itakuwa hewani..This is my second Album..Nimewashirikisha waimbaji mahiri sana ambao wamefanya kazi nzuri sana kwa utukufu wa Mungu..Album inasimamiwa na mtumishi wa Mungu ,producer John Mtangoo..Nahitaji maombi yenu ili kazi ya Mungu iende vizuri..MUNGU AWABARIKI


 Picha za zamani katika albamu yake ya kwanza.
Hapa alikuwa kwenye tamasha akiwa na Yvon Chakachaka wa south Africa na Anastazia Mkahabwa wa Kenya ilikuwa Diamond Jubilee

Hapa akiimba Uwanja wa ndege Dodoma mbele ya waheshimiwa nadhani wote unawajua


 Bonyeza kwenye picha hiyo hapo juu usikilize wimbo mmojawapo katika albamu yake ya kwanza

Blog hii inamtakiwa mafanikio katika maadalizi ya albamu hiyo ya pili.

https://soundcloud.com/martmalecela/hellen-chiwanga

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 4777775 au Whatup, +255 715 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni