Jumatatu, 20 Oktoba 2014

UJIO WA ANGEL BENARD, HII NI KUTOKA IKITO.COM


ANGEL BENARD ni jina ambalo limekuwa likisikika kwa miaka kadhaa sasa kwenye ulimwengu wa muziki wa gospel. Angel Benard mwenye miaka 25 hatimaye sasa anaachia album yake NEW DAY kwenye mfumo wa digitali kupitia Mkito.com. Watu wengi wamekuwa wakisubiri kusikia nyimbo zake za zamani lakini haikuwa rahisi kuzipata. Album hii ni album ya 3 ya mwana dada huyu mwenye sauti ya maajabu. Ni wasanii wachache sana wa muziki wa gospel ambao wamefanikiwa kuvusha nyimbo zao zikapendwa na wapenzi wa gospel pamoja na wapenzi wa muziki wa bongo flava, RnB n.k. na mwimbaji huyu ni mmoja wapo.

Katika kuitambulisha album hii Angel Benard ataachia wimbo mmoja kila siku ya Alhamis kwa wiki 10 mfululizo. Wimbo wa kwanza utatoka tarehe 23 October na unaitwa NEED YOU TO REIGN ukiwa katika minodoko ya Reggae.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 4777775 au Whatup, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Hakuna maoni: