Jumatatu, 7 Aprili 2014

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA ASKOFU WA KANISA LA ANGLICAN CENTRAL TANGANYIKA


  Waziri mkuu Mizengo Pinda na mkewe wakitoa heshima za mwisho walipokuwa wakiuaga mwili wa aliyekuwa Askofu wa kanisa la Anglican Central Tanganika Godfrey Mdimi Mhogolo kabla ya ibada ya mazishi iliyofanyika katika kanisa la roho mtakatifu Dodoma.
  Mjane wa Marehemu aliyekuwa Askofu wa Kanisa la Anglican Central Tanganika Godfey Mhogolo, Iren Mhogolo akiwa mwenye huzuni pembeni ya jeneza kabla ya kuingizwa kaburini.
 Maaskofu mbalimbali wa kanisa la Aglican wakilishusha jeneza lenye mwili wa aliyekuwa  Askofu wa kanisa hilo Central Tanganika Godfrey Mdimi Mhogolo kaburini, katika mazishi yaliyofanyika nje ya kanisa la Roho Mtakatifu maarufu  la Mtungi Mjini Dodoma.
 Maaskofu mbalimbali wa kanisa la Aglican wakiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekuwa Askofu wa kanisa la Anglican Central Tanganika aliyefariki Mwishoni mwa mwezi uliopita alipokuwa kwenye matibabu nchini Africa ya kusini.
 Waziri mkuu Mizengo Pinda akiweka mchanga kwenye kaburi la aliyekuwa Askofu wa kanisa la Anglican Central Tanganika Godfrey Mdimi Mhogolo
 
   Waziri mkuu Mizengo Pinda na mkewe wakiweka shada ya maua juu ya kaburi la aliyekuwa Askofu wa kanisa la Anglican Central Tanganika aliyefariki Mwishoni mwa mwezi uliopita alipokuwa kwenye matibabu nchini Africa ya kusini.
Waziri mkuu wa zamani Edwald Lowasa akiweka shada ya maua juu ya kaburi la aliyekuwa Askofu wa kanisa la Anglican Central Tanganika aliyefariki Mwishoni mwa mwezi uliopita alipokuwa kwenye matibabu nchini Africa ya kusini.
 Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akiweka shada la maua kwenye kaburi hilo.
 Familia ya Marehemu Godfrey Mdimi Mhogolo aliyekuwa Askofu mkuu wa kanisa la Anglicani Central Tanganika wakiwa katika eneo la makaburi ambapo amezikwa nje ya kanisa la Roho Mtakatifu Dodoma
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Hakuna maoni: