Jumanne, 28 Januari 2014

JUMAPILI HII YA TAR 2/02/2014 KANISA LA CITY WORSHIP CENTER KUTIMIZA MWAKA MMOJA UNAKARIBISHWA SANA KWENYE IBADA MAALUMU YA SHUKRANI

  
Kanisa la City Worship Centre lililo chini ya Mchungaji Timothy Mwita linatazamia kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake mapema mwaka jana. Blog yetu ilipata nafasi ya kuongea na Mchungaji huyo Kiongozi wa Kanisa hilo.

Ze Blogger: Mchungaji Kiongozi ninayo furaha kukutana na Wewe, siku ya Leo.

Pastor Mwita: Asante sana nami pia nimefurahi.

Ze Blogger: Tarehe 2 February, 2014 tunategemea nini kutoka City Worship Centre?

Pastor Mwita: Siku ya tarehe 2/2 tunategemea kuwa na Ibada maalum ya maadhimisho (Anniversary) ya mwaka mmoja wa huduma yetu,tangu kuanza kwa kanisa.

Ze Blogger, hongereni sana, kumekuwa na uibukaji wa makanisa kama uyoga siku za miaka ya karibuni na kuna madhehebu makanjanja yamekuwa yakianzishwa kila leo, wewe Kama huduma mpya katika Jiji lenye huduma lukuki hapa Dar-es-Salaam changamoto zipi umekutana nazo kihuduma.

 Pastor Mwita: Changamoto ya kwanza ni utofauti wa mji na miji niliyowahi kufanya huduma kama Mwanza na Knjaro,mji huu watu wake wako busy sana, pia ni rahisi kuwapata washirika wa ktkt ya wiki mikoani sio hapa,pia watu ni watafiti sana na hii inawafanya wachungwe na mch zaidi ya mmoja, mtu anaweza kuja kanisani saa 3 akiwa ameshasali makanisa hata 2 tayari,wengi hawachungwi. Pia yapo maeneo ambayo hayajafikiwa kabisa hapahapa mjini.,na yanahitaji huduma maalum. Eneo la kudumu la kuabudia ni changamoto nyingine to mention the few.

Ze Blogger: Nina amini yeye aliyekuita atakuongoza, siku ya tarehe 2 kutakuwa na nini hasa.

Pastor Mwita:Tarehe 2 kutakuwa na kipindi cha kusifu na kuabudu kwa muda wa kutosha kama desturi ya kanisa letu,pia tutakuwa na wageni tuliowaalika toka maeneo mbalimbali ya jiji na nje ya jiji,pamoja na waimbaji binafsi., hafla yetu itakwenda sambamba na kuwatambua watu waliotusaidia kufikia mafanikio haya. Mwisho tutamaliza kwa kula pamoja. Ibada zetu kwa kawaida huanza saa 3-5, lakini kwa sababu ya umuhimu wa tukio hili tutaanza saa 2-7.
 Ze Blogger: Mtu anawezaje kufika huduma hii ilipo?

Pastor Mwita: Jinsi ya kufika kituo kikuu ni Morocco kisha unaelekea kama unakwenda Mwenge mkono wa kulia kuna Hospitali ya AAR basi nyuma yake ndani ya Shule ya Sunrise mtaa wa Chato- Regent Estate

Ze Blogger: asante sana pastor Mungu akubariki.

Pastor Mwita: Asante ubarikiwe na wewe
 
KWA HISANI YA SAMUEL SASALI

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni