Ijumaa, 15 Novemba 2013

UTANGULIZI KITABU CHA MATHAYO KATIKA AGANO JIPYA

Utangulizi 

Mathayo alikuwa mtoza ushuru ambaye Bwana Yesu alimwita awe mwanafunzi wake mwanzoni kabisa wa huduma yake ya hadharani. Kwa hiyomambo mengi anayoyaelezea aliyashuhudia kwa macho yake mwenyewe.

Anaanza kwa kueleza kwa kirefu kuhusu kuzaliwa kwa Yesu
na Bikira Maria, kubatizwa kwake na kujaribiwa kwake nyikani. Yesu alikuja akihubiri juu ya Ufalme wa Mungu ambao ni wa kila mtu anayetaka kupata uzima wa milele. Mtu anaingia katika Ufalme huu kwa kutubu dhambi na kumwamini Yesu. Mathayo ameyagawa mafundisho ya Yesu katika sehemu kubwa tano: Maadili, Kueneza Habari Njema, Mifano, Ushirika na kuja kwa Ufalme wa Mungu. Sehemu ya Mwisho ya Injili ya Mathayo inaeleza juu ya kufa na kufufuka kwa Yesu, na agizo alilotoa kwa wote wanaomwamini kueneza Habari Njema ulimwenguni kote. Wazo Kuu Shabaha kuu ya Mathayo katika kuandika Injili hii, ilikuwa ni kuonyesha kwamba Bwana Yesu anakamilisha

ahadi aliyoitoa Mungu katika Agano la Kale. Kwa sababu hii, Bwana Yesu anatambulishwa kuwa ni mwana wa Mfalme Daudi na pia mzao wa Abrahamu

(1:1). Kadhalika Mathayo anatumia mifano mingi kutoka katika unabii
uliotolewa na manabii wa Agano la Kale, kueleza maisha ya Bwana Yesu ambaye alikuja kuwa Mwokozi wa Wayahudi

(1:21),wa watu Mataifa mengine

(4:13-16)na hatimaye Mwokozi wa ulimwengu wote

(28:19).Maadili yawapasayo watu wanaoingia katika Ufalme wa Mungu yanaelezwa katika Mahubiri ya Mlimani

(Sura 5-7),ambapo wana wa Mungu wanaagizwa kukataa kufuata maad

ili ya dunia hii na kutafuta kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake, ndipo hayo mengineyo watakapozidishiwa

. (6:33). Mgawanyo

1 Maisha na huduma ya Bwana Yesu (1:1-4:25)

2 Mahubiri ya Mlimani (5:1-7:29)

3 Mafundisho, Mifano na Mazungumzo (8:1-18:35)

4 Safari ya kwenda Yerusalemu na maonyo ya mwisho (19:1-23:39)

5 Unabii kuhusu mambo yajayo (24:1-25:46)

6 Kufa na kufufuka kwa Bwana Yesu (26:1-28:20)

Hakuna maoni: