Jumatatu, 18 Novemba 2013

UTANGULIZI KITABU CHA INJILI CHA MARKO KATIKA BIBLIA


Marko ambaye aliitwa Yohana Marko a lifuatana na Mtume Paulo katika safari zake za kitume.Huyu ndiye anayetajwa na mababa wa kanisa Papiass, Irenio na Klement wa Aleksandria kuwa mshirika wakaribu sana wa Mtume Petro.Uhusiano huu wa karibu na Petro umeonyeshwa katika(1Pet..5:13), 
 
pale ambapo Petro anamtaja Marko kama “mwanawe.” Hatimaye aliishi
Rumi ambako aliandika kumbukumbu zaMtume Petro. Kwa hiyo Injili ya
Marko inawakilisha maneno ya mtu aliyeshuhudia kwa macho yake mwenyewe juu ya maisha ya Yesu yanayoelezwa katika Injili hii. Yohana Marko ni mtoto wa Maria ambaye nyumbani

kwao kulikuwa Yerusalemu, ambako kunaonekana kuwa kituo kikuu cha Ukristo
(Mdo. 12: 12). Marko alisafiri na Barnaba ambaye ni mjomba wake mpendwa
(Mdo. 4:36 -37 )kwenda Antiokia ya Syria (Mdo 12:25) ambako walifuatana na Paulo kwenye safari yake ya kwanza ya kitume.Marko hata hivyo aliwaacha Barnaba na Paulo huko Kipro na kurudi Yerusalemu (Mdo 13:13) Baadaye Barnaba na Marko walielekea Kipro wakati Paulo akienda Asia. Miaka kumi baadaye ( 60 B.K)
Marko alikuwa pamoja na Paulo huko Rumi (2Tim.4:11; Kol.4:10.)Shabaha ya Marko ilikuwa ni kukusanya pamoja ujumbe wote wa Injili. Kwa sababu hii, Injili ya Marko inakazia 

zaidi matendo ya Yesu kuliko maneno Yake. Pia Injili hii inatumia nafasi kubwa kueleza matukio ya juma la mwisho la maisha ya Bwana Yesu. Marko anaanza kwa kueleza habari za huduma ya Bwana Yesu hadharani na juu ya kuhubiri Kwake kuhusu Habari Njema ya Ufalme wa Mungu. Kisha anatoa unabii wazi kuhusu matazamio ya kifo cha Bwana Yesu
(Mk. 8:31;9:31;10:33-34,45).Hatimaye anaeleza jinsi Bwana Yesu alivyosulibiwa msalabani kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, kufufuka Kwake kutoka kwa wafu, kuonekana Kwake nawanafunzi Wake baada ya kufufuka, maneno na maagizo Yake ya mwisho na kupaa Kwake kwenda mbinguni. Tarehe Inawezekana ni katika wakati huu wa uhai wa Petro, au muda mfupi tu baada ya kifo chake (55-65 B.K.), ambao Marko aliandika Injili hii yenye kuchukua jina lake. Wazo Kuu 

Marko anamdhihirisha Bwana Yesu kuwa ni Mtumishi wa Mungu, Mtu wa vitendo, aliyekuja kutimiza mapenzi ya Mungu. Marko anaonyesha waziwazi huduma ya Yesu na utendaji Wake wa miujiza, uponyaji Wake, mamlaka Yake juu ya pepo wachafu na nguvu Zake, Bwana Yesu alithibitishwa kuwa si mtumishi wakawaida bali kwamba kwa hakika alikuwa Mwana wa Mungu.Ufufuo wa Yesu ulithibitisha yale yote aliyotenda na sasatunangojea kurudi 

Kwake kwa utukufu, kutoka mbinguni. Marko aliandika Injili hii ili pia kuwatia moyo Wakristo walioishi Rumi wakati wa mateso. 


Mgawanyo 
Yohana Mbatizaji na ubatizo wa Bwana Yesu (1:1-13)
Huduma ya Yesu Galilaya (1:14-9:50)
Safari ya kwenda Yerusalemu na kuingia mjini (10:1-11:25[26])
Matatizo mjini Yerusalemu (11:27-12:44)
Unabii kuhusu mambo yajayo (13:1 -37)
Kufa kwa Yesu na kufufuka kwake. (14:1-16:8[9-20])

Hakuna maoni: