Hata hivyo, hakusita kueleza wazi kuwa baadhi
ya mazingira yanawakatisha tamaa katika huduma hiyo na kusababisha
waimbaji wengine kufikia uamuzi wa kupanga bei kama ilivyo kwa waimbaji
wa nyimbo za mataifa
Nikitaja wimbo wa ‘Nasubiria baraka’ itakuwa
rahisi kutambua mapema ninayemzungumzia katika safu hii kwani wimbo huo
umeokea umesambaa na kujulikana ndani na nje ya nchi.
Dada huyu anaitwa Christina Mbilinyi (28), aliye
na kipaji cha uimbaji alichokirimiwa na Mungu. Mashabiki wa nyimbo za
Injili wanaposikia wimbo huo mara nyingi husimama na kucheza kwani
unakubalika na kugusa maisha ya watu.
Kwa mara ya kwanza alipoanza kusikika masikioni
kwa Watanzania, wengi walidhani dada huyu ni Mkenya kutokana na
mpangilio wa mashairi na ladha ya uimbaji wake.
Msanii huyo amefanikiwa kushiriki mialiko mingi
kwa ndani na nje ya nchi tangu alipotoa albamu ya wimbo huo mwaka 2011,
amekuwa pekee kabla ya kumpata meneja aliyenaye kwa sasa.
Habari mpya kutoka kwa Christina ni sauti yake
anayoipaza kwa waimbaji wa muziki wa Injili akionya uimbaji wa nyimbo
hizo kutumika zaidi kama biashara.
“Sheria ya Mungu ni ngumu sana, Neno lake linasema
walioitwa ni wengi ila watenda kazi ni wachache. Wengine wanafanya
huduma kutoka ndani ya mioyo yao, wengine wanatanguliza sana pesa, wako
kimasilahi zaidi, hiyo haipendezi,” anasema Christina.
Anafafanua kuwa kuna tofauti kati ya kuingia
makubaliano na kuchangiwa gharama za mwaliko; “Hilo linaeleweka, siyo
lahisi kumwita mwimbaji bila kumwandalia nauli au marejesho ya gharama
alizotumia kufika katika eneo hilo la huduma.”
Hata hivyo, hakusita kueleza wazi kuwa baadhi ya
mazingira yanawakatisha tamaa katika huduma hiyo na kusababisha waimbaji
wengine kufikia uamuzi wa kupanga bei kama ilivyo kwa waimbaji wa
nyimbo za mataifa.
Christina ambaye kwa sasa anatarajia kuipua albamu
yake mpya itakayojulikana kwa jina la ‘Mtazamo wako’ , ni muumini wa
Kikristo anayesali na kufanya huduma katika Kanisa la Mito ya Baraka
lililopo Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Christina anajivunia mafanikio kwa kufahamika na
kupata ushirikiano mzuri katika jamii pamoja na kuona watu wakipata
baraka na faraja kupitia kazi yake ya uimbaji.
“Masuala ya mali ni ahadi tulizopewa, zipo tu zinakuja kwa wingi, maana amenibariki,”anasema Christi
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671
AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni