Jumanne, 7 Mei 2013

PINDA ALIPOTEMBELEA KANISA LA OLASITI NA MAJERUHI KWENYE HOSPITALI YA MKOA WA ARUSHA, MT. MERU KUFWATIA MLIPUKO WA BOMU ULIYOTOKEA ARUSHA JUMAPILI


 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiangalia sehemu lilipodondoshwa bomu hilo.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Viongozi na Waumini wa Kanisa Katoliki la Olasiti Jijini Arusha May 7,2013 alikokwenda kutoa pole kufuatia mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono uliotokea kanisani hapo May 6,2013 na kusababisha vifo na majeruhi.

Paroko wa Kanisa Katoliki la Olasiti la Arusha Peddy Castelino akiomba wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipotembelea kanisa hilo May 7,2013 kutoa pole kufuatia mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono uliotokea kanisani hapo May 6,2013 na kusabisha vifo na majeruhi.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Paroko wa Kanisa Katoliki la Olasiti jijini Arusha, Peddy Castelino (kulia) May 7,2013 wakati alipotembelea kanisa hilo May 6,2013 ambako ulitokea mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono na kusababisha vifo na majeruhi.

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na kumpa pole Askofu wa Jimbo Kuu la Arusha, Mhashamu Josephat Lebulu

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na kumpa pole Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu, Francisco Montecillo

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapa Pole Askofu wa Jimbo Kuu la Arusha, Mhashamu Josephat Lebulu (kushoto ) na Balozi wa Vatican nchini, Askofu Mkuu, Francisco Montecillo (katikati), May 7,2013 baada ya kutembelea Kanisa Katoliki la Olasiti jijini Arusha ambako May 6,2013 ulitokea mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono na kusababisha vifo na majeruhi.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapa pole baadhi ya majeruhi wa bomu la kutupwa kwa mkono lililolipuka katika kanosa Katoliki la Olasiti Arusha wakati alipowatembelea kwenye hospitali ya mkoa wa wa Arusha, Mount Meru, May 8,2013.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni