Jumanne, 7 Mei 2013

TANESCO NDIYO CHANZO CHA MAONO MAPYA YA HUDUMA YA KIMATAIFA YA ASKOFU ZAKARY KAKOBE

 TUNAISHUKURU SANA TANESKO KWA KUIWEZESHA HUDUMA YA ASKOFU ZAKARY KAKOBE KUPANDA NGAZI. HAYA NI MANENO ALIYOZUNGUMZA ASKOFU ZACHARY KAKOBE SIKU YA JUMAPILI YA TAREHE 22, JULAI 2012. ALIYAZUNGUMZA SIKU YA KUWEKA WAKFU MITANDAO YA INTERNET YA HUDUMA YAKE YA KIMATAIFA.

 ALISEMA KUWA TATIZO LILILOKUWEPO KATI YAKE (KANISA) NA SERIKALI (TANESKO) ULIKUWA NI MPANGO WA MUNGU. MUNGU HAKUTAKA KANISA LA FGBF WAWEKE MTANDAO WA TELEVISION KWA JINA LA HOLNES TELEVISION KAMA ILIVYOTARAJIWA. KWA MAOMBI YALIYOANZA TAREHE 29/03/2010 AMBAYO HATA SASA YAKIENDELEA NDIYO YALIYOTOA JIBU KAMILI LA MPANGO WA MUNGU KWA HUDUMA HIYO YA ASKOFU KAKOBE. MUNGU ALIWEZA KUJIBU MAOMBI KWA KUZUIA UMEME KUPITA KAMA ILIVYOKUWA KWA NABII ELIYA ALIYESIMAMISHA MVUA KWA MIAKA MITATU NA NUSU (YAKOBO 5:17-18).

ASKOFU AKIFUNDISHA KANISANI HAPO MAKAO MAKUU YA KANISA MWAKA 2010 ALISEMA KUWA UMEME KAUFUNGA NA HAKUNA WA KUFUNGUA ( ISAYA 22:22) MPAKA YEYE MWENYEWE AUFUNGUE KWA MAOMBI. MAOMBI YA KUZUIA UMEME KUPITA YALIANZA BAADA YA SERIKALI KUAMUA KUPITISHA NGUZO ZA UMEME WA MSONGO KWA NGUVU KUBWA YA DOLA BILA MWAFAKA KUFIKIWA BAINA YA ASKOFU NA SERIKALI. BAADA YA ASKOFU KAKOBE KUONA POLISI NA SILAHA ZAO, WAKIWA TAYARI KUPAMBANA NA WATU WA MUNGU. YEYE ALIWAOMBA KUINGIA KANISANI TAYARI KWA KUANZA KAMBI YA MAOMBI MPAKA KIELEWEKE.

KANISA HILO LA FULL GOSPEL BIBLE FELLOWSHIP, LIMEKUWA KATIKA MAOMBI MAZITO, MAOMBI KAMA KAZI KWA AJILI YA KUOMBEA ULIMWENGU NA MSINGI MKUBWA WA MAOMBI UKIWA KATIKA ( ZABURI 2:8 ). MAOMBI HAYO YALIKIGUSA KITI CHA MUNGU NA TAREHE 16, APRILI 2012, ASKOFU KAKOBE ALITOKEWA NA YESU KRISTO MWENYEWE NA KUMKABIDHI BUNDA LA FUNGUO ZA ULIMWENGU (ZABURI 2:8). TUNAWASHUKURU SANA TANESKO NA SERIKALI KWA UJUMLA KWA KUTUWEZESHA KUPANDA NGAZI, HAYO NI MANENO YA ASKOFU MWENYEWE. TUMEPANDA NGAZI KUTOKA KUTTUMIKA HAPAHAPA TU SASA TUNAUENDEA ULIMWENGU MZIMA ( DUNIA NZIMA ).. MWAKA HUU HUDUMA YA KIMATAIFA YA ASKOFU ZACHARY KAKOBE IMEANDAA KONGAMANO KUBWA SANA LA KIMATAIFA LITAKALOFANYIKA NCHINI CANADA. KONGAMANO HILO LITAFANYIKA KUANZIA TAREHE 20 HADI 23 YA MWEZI WA SITA 2013.

 KWA MAELEZO ZAIDI INGIA HAPA WWW.bishopzacharykakobe.org. ASKOFU KAKOBE ANAPATIKANA KATIKA MITANDAO IFUATAYO. WWW.bishopzacharykakobe.org, WWW.fgbfchurch.org. NDANI, YA MITANDAO HII UNAWEZA KUONA MITANDAO MINGINE YA KIJAMII KAMA FACEBOOK, TWITTWER, MY SPACE, GOOGLE NA YOUTUBE YENYE VIDEO NYINGI ZA MATENDO MAKUU YA MUNGU. KUNA SHUHUDA MOTOMOTO KAMA VILE ZA WATU WALIOPONYWA UKIMWI MARA TU BAADA YA KUOMBEWA NA ASKOFU ZACHARY KAKOBE. SHUHUDA HIZO ZIMETHIBITISHWA KISAYANSI KATIKA HOSPITALI KUBWA NA ZINAZOAMINIKA NCHINI TANZANIA. HAKIKA MUNGU NDIYE

ANAYELITHIBITISHA NENO LA MTUMISHI WAKE KWA ISHARA NA MIUJIZA MIKUBWA (MARKO 16:20). OLE NI KWA MWANADAMU ANAYEUPIGA MATEKE MCHOKOO!! ASHINDANAE NA BWANA ATAPONDWA KABISA.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni