Jumatano, 24 Aprili 2013

GLORIOUS CELEBRATION WAFANYA FAMILY DINNER PARTY. ILIWAKUTANISHA NA WANAFAMILIA WAO


Usiku wa Jumamosi ya tar. 20/04/2013 ulikuwa ni usiku wa GLORIOUS CELEBRATION - Family Dinner. Kusudi kubwa lilikuwa ni kukutana na waimbaji wote wa GC kwa pamoja na wazazi wao, walezi na ndugu wa karibu. Hii pia ilijumuisha wanandoa kwa wana GC amabao wameoa au kuolewa.

Kwanza tunamshukuru Mungu kwa kibali na yote yaliyojiri. Pili tunamshukuru mlezi na mbeba maono wa GC, wazazi na wote waliofika. Kwa nyakati tofauti, mlezi wetu pamoja na baadhi ya wazazi walitoa mahusia mbalimbali. Kwa hakika ulikuwa usiku wa furaha kuwaona wanaGC kuwa pamoja na wazazi wao, ndugu jamaa na marafiki.

Ni matumaini yetu siku si nyingi tutakuwa na usiku wa wanaGC wote, yaaani pamoja na wewe. "Tazama jinsi ilivyo vema na kupendeza ndugu wakikaa pamoja kwa umoja ni kama mafuta mafuta mazuri yatiririkayo kichwani mpaka kwenye ndevu za haruni" Zaburi 133:1-2.

SIFA NA UTUKUFU KWA MUNGU!
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni