Jumanne, 2 Aprili 2013

BAADA YA KUTOKUREKODI MATOLEO MAWILI YALIYOPITA SOLOLISTI WA KWETU PAZURI AJA KIVINGINE





Yvonne Umulisa wa Ambassadors of Christ ya Rwanda

MWIMBAJI maarufu wa kwaya ya Ambassadors of Christ ya Kanisa la Waadventista wa Sabato la mjini Kigali, Rwanda, Yvonne Umulisa, ameibuka tena katika albamu mpya ya kwaya hiyo baada ya kukosekana katika matoleo matatu mfululizo.

Umulisa ambaye alitamba na wimbo wa Kwetu Pazuri akiwa mwimbaji mwanzilishi na kujipatia umaarufu mkubwa, aliondoka katika kwaya hiyo kwa muda baada ya kufunga ndoa miezi michache baada ya kunusurika katika ajali ya gari.

Baada ya kukosekana katika albamu tatu za kwaya hiyo, hatimaye ameibuka tena katika albamu mpya namba 8 iitwayo Kaeni Macho. Katika albamu hiyo, Umulisa anatamba na wimbo Twawona Okuswala (Tumeepushwa Aibu), wimbo huo umeimbwa kwa lugha ya Kiganda.

Katika wimbo huo unaoanza kwa kibwagizo, Umulisa anaonekana akiongoza kuimba ubeti wa kwanza kwa hisia kali na kwa umahiri mkubwa akitoa sauti yenye mvuto kama alivyoimba katika wimbo wa Kwetu Pazuri.

Umulisa  akiwa Kigali alisema kuwa anajisikia furaha sana kurejea katika kwaya yake hiyo na kuungana tena na mashahabiki wake kupitia huduma ya uimbaji.

Kuhusu siri ya kuendelea kufanya vizuri katika uimbaji kwenye albamu hiyo alisema: "Mimi napenda sana kuimba, hivyo ninafanya kitu ninachokipenda. Siwezi kujua kiwango changu kikoje, ila wasikilizaji ndio wanaweza kujua."
Akizungumzia kiwango cha mwimbaji huyo baada ya kurejea tena katika huduma hiyo, Mwalimu wake, Ssozi Joramu, alisema kuwa Umulisa ni balaa.

"Yule dada ni balaa. Inashangaza, mtu aliyekaa muda wote ule bila mazoezi lakini hajapoteza kiwango,"alisema Ssozi.

Umulisa aliachana na kwaya hiyo kwa muda alipofunga ndoa miezi michache tu baada ya kunusurika katika ajali ya gari iliyolikumba kundi hilo wakati wakirejea kwao kutoka Dar es Salaam, ilikuwa Mei 9, 2011.

Waimbaji wenzake watatu walifariki dunia na wengine kadhaa wakajeruhiwa vibaya.

Aliolewa mjini Gisenyi huko kwao jambo lililomfanya asimame kwa muda kuimbia kwaya hiyo. Sasa amehamia tena Kigali na mumewe.

Pia hakuweza kushiriki katika matoleo matatu ya albamu za kwaya hiyo yaliyofautia, wala katika safari za kwaya hiyo zilizofuatia, jambo lililowafanya mashahabiki wake waliokuwa na hamu ya kumuona waulize maswali mengi.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

It is perfect time to make some plans for the future and it
is time to be happy. I have read this post and if I could I wish to suggest you few interesting things or advice.
Perhaps you can write next articles referring to this article.
I desire to read even more things about it!

Also visit my web-site - Juegos Online Gratis

Bila jina alisema ...

Your method of explaining everything in this paragraph is actually nice,
every one be capable of effortlessly understand it, Thanks a lot.



Feel free to visit my blog - bancuri deocheate noi