Jumamosi, 30 Machi 2013

KWA NINI TUNASHEREHEKEA PASAKA INAMAANA GANI KWETU


                     
Pasaka ni sikuku iliyoamriwa na Mungu tangu siku za kale
kwa wayahudi kuifanya katika mwezi wa Abibu au Nisani
katika “kalenda ya kiebrania” yaani mwezi wa 3 au 4 katika
kalenda ya kirumi, kwa lengo la kumbuka njisi Mungu
alivyowakomboa kutoka utumwani Misri; Twasoma:
“Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie pasaka BWANA,
Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku BWANA; Mungu wako. Nawe umchinjie pasaka BWANA, Mungu wako katika kundi la kondoo na la ng’ombe, mahali atakapochagua BWANA apakalishe jina
lake.” (Kumbukumbu 16:1-2) Soma pia: (Kutoka 12:14)
Kama tulivyoona katika pasaka wayahudi waliamriwa
kuchinja mnyama mmoja katika kundi, lakini
tunapoendela kusoma tunaona jinsia Mungu alivyoamuru
mnyama huyo aokwe na kuliwa; Twasoma:

 “Usimle pamoja na mikate iliyotiwa chachu; siku saba
utakula naye mikate isiyotiwa chachu, nayo ni mikate ya
mateso; kwa maana ulitoka nchi ya Misri kwa haraka; ili
upate kukumbuka siku uliyotoa nchi ya Misri, siku zote za
maisha yako. Wala isionekane kwako chachu muda wa
siku saba katika mipaka yako yote; wala katika hiyo
nyama uchinjayo siku ya kwanza jioni, kisilale cho chote
usiku kucha hata asubuhi. Usimchinje pasaka ndani ya
malango yako yote akupayo BWANA, Mungu wako; ila
mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako apakalishe
jina lake, ndipo mtakapomchinjia pasaka jioni, katika
machweo ya jua, kwa wakati kama uliotoka
Misri.” (Kumbukumbu 16:3-6); Soma pia: (Kut 12:3-13)
Katika mwezi huo wa abibu ambao Mungu aliufanya kuwa
mwezi wa kwanza kwako, Wayahudi walifanya karamu ya
Pasaka kuwa kumbukumbu la jinsi Mungu alivyowaokoa
kutoka Misri (Kutoka 12:1-51; Walawi. 23:5).

Pasaka maana yake ni "kupita Juu", maana Mungu alipita
juu ya nyumba zao asiwaangamize wazaliwa wao wa
kwanza; Twasoma:
“Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba
mtakazo kuwapo; nami nitakapoiona ile damu, nitapita
juu yenu, lisiwapate pigo lo lote likawaharibu nitakapoipiga nchi ya Misri.” (Kutoka 12:13); Soma pia:(Kutoka 12:27)

JE? WAISRAELI WALIKUWA NA SIKUKUU ZINGINE ZAIDI YA PASAKA.
Biblia inaeleza wazi ya kuwa wayahudi walikuwa na sikukuu zingine ambazo Mungu aliwaagiza mbali pasaka;
basi hebu tuzione sikukuu hizo;

PENTEKOSTE - Pentekoste maana yake ni 50, Sikukuu hii
ilikuja siku ya 50 baada ya Pasaka. Pentekoste iliitwa pia
Karamu ya Juma, maana Mungu aliwaamuru wajihesabu
juma saba kuanza baada ya Pasaka. Hivyo, karamu hiyo ilitokea mwezi wa 6. Siku ya Pentekoste Wayahudi walimtolea Mungu mikate ya ngano miwili iliyopikwa kutokana na mazao yao ya kwanza. (Walawi 23:15-22)

KARAMU YA VIBANDA - Sikukuu hii ilitokea mwezi wa 10.
Kwa muda wa siku saba walikaa katika vibanda wakikumbuka jinsi Mungu alivyowalisha na kuwatunza jangwani walipotoka Misri. Nao wakamtolea Mungu shukrani kwa mavuno yao(Walawi 23:39-43).

SIKU YA UPATANISHO. Mara moja kila mwaka (terehe 10
mwezi wa 10) kuhani mkuu aliingia Patakatifu pa Patakatifu.
Humo aliweka damu juu ya Kiti cha Rehema (funiko la Sanduku la Agano) kusudi dhambi za Wayahudi zisahauliwe na Mungu kwa muda wa mwaka mmoja (Walawi 16:1-
34; 23:27-32), Wayahudi walijinyima chakula kuonyesha huzuni kwa dhambi zao na kujinyenyekea kwa Mungu.

JE SIKUKUU HIZI ZA WAISRAELI IKIWEMO PASAKA ZINAENEDELEA?
Neno la Mungu linaeleza wazi ya kuwa sikukuu hizi za kale
zilikomeshwa na Mungu alitupa utaratibu mwingine wa jinsi
alivyotaka tuenende; Twasoma:
“Tena nitakomesha furaha yake yote, na sikukuu zake, na
siku zake za mwandamo wa mwezi, na sabato zake, na
makusanyiko yake yote yaliyoamriwa.” (Hosea 2:11)
“Angalia, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapofanya
agano jipya na nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda. Si
kwa mfano wa agano lile nililofanya na baba zao, katika
siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nalikuwa
mume kwao, asema BWANA.”(Yeremia 31:31-32)

JE WAKRISTO TUNA PASAKA LEO?
Ni kweli wakristo tuna pasaka leo, walakini si katika utaratibu ule uliotumika katika siku za waisraeli, kama tulivyoshuudia maandiko yaneleza wazi ya kuwa sikukuu hizo zilikomeshwa; Basi hebu tuone utaratibu wa Pasaka ya
wakristo leo ni upi;
Zingatia: Kama tulivyoona hapo juu, waisraeli waliokolewa na damu ya mnyama walio ipaka katika miimo na miisho ya milango yao na ndipo malaika wa Bwana alipotambua na kupita juu; Soma tena: (Kutoka 12:13, 27); lakini wakristo tunaambiwa pasaka wetu ni Yesu mwenyewe aliyetuokoa kwa damu yake; Twasoma:
“Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema,
Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhamb
ya ulimwengu!” (Yohana 1:29); Soma pia: (Yohana 1:36)
“Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika
mwenendo wenu usiofaa milioupokea kwa baba zenu;
bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo
asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.” (1 Petro 1-18-19)
“Basi jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mapate kuwa
donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa
maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka,
yaani, Kristo;” (1 Wakoritho 5:7)

Basi kama tulivyoona Neno la Mungu linatuthibitishia ya
kuwa kwa sasa wakristo tunaokolewa na damu ya Yesu
ambaye ndiye Pasaka wetu na si kwa damu ya mnyama
aliyekuwa Pasaka wa kale. Basi kiwa hivyo ndivyo, ni dhahiri hata utratibu wa kusherehekea pasaka kwa wakristo ni tofauti, Basi hebu tuone wakristo tunasherehekeaje pasaka yetu leo.

Yesu alipokuwa akila Pasaka ya mwisho pamoja na wanafunzi wake, aligeuza Pasaka. Aliwaambia kwamba, kuanza siku ile, watakapokula mikate wangekumbuka mwili wake uliotolewa kwa ajili yao badala ya kukumbuka kuokolewa kutoka utumwani nchini Misri; Twasoma:
“Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki,
akaumega akawapa wanafunzi wake, akisema, Twaeni mle;
huu ndio mwili wangu 

Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.” (Mathayo 26:26-28)
“Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa ninyi,
ya kuwa usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, na ye akiisha
kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio
kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi
hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, kikombe
hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kwa kila
mywapo, kwa ukumbusho wangu. Maana kila mwulapo
mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti
ya Bwana hata ajapo.” (1 Wakorintho 11:23-26).


JE WANAOSHEREHEKEA PASAKA YA KALE WAMEPOTEA?
Ni kweli karibu ulimwengu mzima unasherehekea pasaka
kama walivyokuwa wakisherehekea wayahidi nyakati zile,
wakidhani ndivyo ilivyo agizwa, basi na tuzingatie maneno
yafuatayo; Twasoma:
“Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini
mwisho wake ni njia za mauti” (Mithali 14:12)
“Akajibu, akasema, Kila pando asilolipanda Baba yangu
wa mbinguni litang’olewa. Waacheni hao ni viongozi vipofu
wa vipofu. Na kipofu akimwongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.” (Mathayo 15:13-14)
 “Si kila aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika
ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya
Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile,
Bwana, Bwana hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa
jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza
mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi
kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao
maovu.” (Mathayo 7:21-23)
 “Basi ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa
mimi na Apolo kwa ajili yenu ili kwamba kwa mfano wetu
mpate kujifunza kutokupita yale yaliyoandikwa; ili
mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha
mwenziwe.” (1 Wakorintho 4:6)

Basi kama tulivyoona, upotofu uliopo katika sikukuu hii ya
pasaka na jinsi Mungu anavyo tuonya kuwa makini na
mafundisho ya uongo, ni dhahiri tunawajibu wa kujifunza
neno la Mungu kwa bidii ili tupate kujua yaliyo mapenzi
yake tukayafanye; Soma: (Yakobo 1:22-25)

Hakuna maoni: