Ijumaa, 7 Desemba 2012

UZINDUZI WA VIDEO YA NITETEE YA DP NI JUMAPILI HII

 Ule uzinduzi uliokuwa ukisubiliwa kwa hamu wa albamu ya 'nitetee bwana' kutoka kwa muimbaji wa nyimbo za injili ambayepia ni mtangazaji wa kipindi cha power drive na gospel fleva katika radio ya praise power anafahamika kwa jina la Deoglas Pius a.k.a DP

Uzinduzi huo utafanyika jumapili hii ya tarehe 9/12/2012 katika kanisa la akuzamu international lililopo posta mpya jengo la ips kabla ya sanamu la posta
Dp amesema kuwa siku hiyo hapatakuwa na kiingilio chochote bali ni bure kabisa hivyo watu wote anawakaribisha katika uzinduzi wake ambao utaanza saa nane mchana na kuendelea

                                                Dp aliyevaa shati jekundu


Pia Dp amewataja baadhi ya waimbaji wa nyimbo za injili watakaomsindikiza kuwa ni


Rungu la Yesu pamoja na kundi lake la ZE GOD'S CHOSEN RAPPERZ wakiwemo Sir mbezi jr na Preacher gazuko

                                          Brian mwimba na kundi lake la Born winners


                                       Frola na Emanuel mbasha pamoja na kundi lao

                         Christina mbilinyi kutoka mkoani mbeya atakuwepo na kundi lake zima
Dp amesemakuwa pia kutakuwa na watu mbali mbali maarufu kama vile team ya Bongo movie akiwepo

Dotnata kwani licha ya kuhudhuria vile vile atahudumu kwa njia ya uimbaji pia Dp amesema watakuwepo pia wasanii wanaoimba muziki wa kidunia wakishuhudia jinsi vijana wanavyomuimbia bwana kama vile kundi zima la wagosi wakaya akiwemo mkoloni

picha hii ikimuonyesha mkoloni kutoka katika kundi la Wagosi wakaya
Mwisho Dp amesemakuwa anawakaribisha watu warika,kabila na dini zote katika uzinduzi.


habari hii kwa hisani ya Preacher gazuko

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni