Jumatano, 5 Desemba 2012

PAPAA WA SEBENE SAMUEL SASALI KIJANA MWENYE MAONO MAKUBWA KATIKA SHAMBA LA BWANA, HUMKOSI FoF,CUMPASS NIGHT NA MATAMASHA MBALIMBALI. MPANGO WAKE NI KUFUTA MATAMASHA YA FIESTA. MWAKA HUU ALIPANGA KUWALETA JOYERS SELEBRATION .

Vijana wengi wa mkoa wa Dar, Tanzania kote na Duniani. si wageni kusikia jina Samuel Sasali  aka Papaa wa sebene, anamiliki blog ya kikristo yenye wasomaji wengi Duniani na wengine wamefuata nyayo zake kwa kuanzisha blog zao, ni kijana ambaye amekuwa akishiriki kwenye matamasha mengi makubwa, kama Afwelo, FOF, Cumpass night, amekuwa ni Mc katika sherehe mbalimbali hata mimi harusi yangu iliyofungwa miaka 6 iliyopita Mc alikuwa Samuel enzi hizo akiwa bado kijana mbichi kabisa. blog hii ilifanya mahojiano kuweza kujua mambo mbalimbali ikiwa lile la mpango wake wa kuwaleta baadhi ya wana Jouyer's celebration kutoka South Afrika fuatana nami katika mahojiano haya utajua nini amesema
Blogger Samuel
  • Martin Malecela

    Shalom mwanzoni mwa mwaka uliahidi kuwaleta baadhi ya wana Joyers imeishia wapi
  • Samuel Sasali

    Tatizo kubwa ni Fedha na Makubaliano ya Msingi
    na Nilikosa muda wa kutafuta wadhamini
    Ila mpaka leo tunachat
  • Martin Malecela

    kwahiyo kama kuja ni mwakani na si mwaka huu siyo
  • Samuel Sasali

    Yap sababu kuna isue kama tatu zikikaa sawa naachana na ajira ya kuajiriwa na bepari na mimi nakuwa bepari hapo ndipo nitaweza
  • Martin Malecela

    ok mwaka huu mmefanya matamasha mfurulizo katika mikoa mbali mbali nafikiri itafuata Mbeya, Singida na sasa mtaenda Moro nk waratibu wakuu wa matamasha haya ni nani na wadhani ni akina nani
  • Samuel Sasali
    Wadhamini ni tofauti tofauti
    Lakini ni Kanisa VCCT na Makanisa wenyeji wa kule tunakokwenda mfano mbeya walikuwa RICC na Singida kwa Pastor Mwakitalima na Morogoro. Ni Mtokambali
  • Martin Malecela

    ok naona speed mnayokwenda nayo ni kali je mna mpango wa kufuta nyayo za fiesta?
  • Samuel Sasali

    Hiyo ndiyo plan
  • Martin Malecela
    changamoto gani ambazo mnakutana nazo mpaka sasa ambazo uafikiri labda wakitokea watu kuwasaidia inaweza ikaongeza speed ya hiyo huduma
    Moja ya kazi anazozifanya ni u mc kwenye shughuli mbalimbali
  • Samuel Sasali
    1. Finances sababu inatugharimu kuwasafirisha wanafunzi
     2. Fiances kwenye Publicity
    3. PA System sababu we need to have our own PA and stage
     4. Cooperation kutoka makanisa mengine maana wanachukulia hiki kitu cha kanisa fulani
     5. Transport most tunazunguka na mabasi au min bus za kukodi...kwa Ujumla wake Fedha ni Jawabu la Mambo yote
  • Martin Malecela
    kuna makampuni yanayotoa udhamini katika mambo mengi kama makampuni ya simu na makampuni ya vInywaji baridi je? mumewahi waza au kujaribu kuwaomba ili kupata udhamini maana najua wanaweza kujitangaza kupitia huduma yenu.
  • Samuel Sasali
    Makampuni mengi ya siku hayana interest na mambo ya kidini tumejaribu kwenda lakini response yao imekuwa ya kujivuta

  • Martin Malecela
    kuna FOF na Campus Night ambavyo vyote mmekuwa mkivifanya kwanza mtu ambaye hajui hivi vitu unaweza kueleza tofauti yake na makusudi ya hivyo vitu viwili
    Baadhi ya waandaaji wa FoF
  • Samuel Sasali
    FoF ni entertainment event and Networking Campus Night ni maalumu kwa ajili ya wanafunzi kwa ujumla
    FoF ni Kila Mwezi Campus Night Mara moja kwa mwaka katika mkoa husika.

  • Martin Malecela

    je FOF ukiacha burudani kunakuwa na nini vitu vingine hasa ukiangalia malika kuna watoto vijana na wazee je yapo mambo ya kuwalenga wote au kuna watu maalumu ambao inawahusu

  • Samuel Sasali

    Kuna Business Presentations, Kuna dinner, Kuna, Uimbaji wa nyimbo za Injili, Kuna games, Kuna comedy, kuna Life sharing experiance (shushuda) etc

  • Martin Malecela

    sasa hivi mko kwenye maandalizi ya FoF Extravaganza ninafikiri ndiyo itakuwa FOF ya mwisho kwa mwaka huu 2012. kwa wale wanao hudhuria wategeme nini na je? kwa wale ambao hawajawahi kufika kabisa kwenye FOF una lipi la kuwaambia ili liwashawishi kufika.
  • Samuel Sasali

    Kwanza kwa Mara ya kwanza tumewaleta Glorious ambao kama Glorious hawajawahi kuja so tumekuja new flevors za muziki, Flora Mbasha and Shusho, Pia watarajie kitu cha tofauti Upande wa Burudani sababu tunafanya full burudani, pia. Watarajie games mpya kabisa na Kitu cha Mwisho ni kwamba FoF imeshusha bei  ni sh 15,000 tu ila safari hii watu watajinunulia chakula
    Tangazo la FoF ya mwisho kwa mwaka huu
  • Martin Malecela
    mmejipanga vipi kwa ajiri ya mwakani
  • Samuel Sasali
    Kwenye nn FoF ama?

    Martin Malecela
  • Huduma zote unazofanya FoF, cumpas Nights n.k
  • Samuel Sasali
    Ndugu mwandishi kwanza nikutofautishie jambo moja, Campus night Iko chini ya VCCT, na FoF haiko chini ya Kanisani ni sehemu ya kazi za FoF Committee. Kuhusu kujipanga Campus Night nisiwe msemaji wa VCCT sababu iko chini ya Campus Ministry, kwenye FoF tumejipanga mpaka mwaka unaisha tuwe kwenye mikoa 10 Tanzania bara na Event Moja Zanzibar sababu FoF. Ni Kila mwezi

  • Martin Malecela
    Asante kwa ushirikiano wako. swali la kizushi najua wengi wangependa kufahamu unaoa lini
  • Samuel Sasali
    Ninaona Mwakani katikati ya mwezi wa 10-12.

    Pamoja na hayo mengi umefahamu kuhusu Samuel pia ni mwalimu mzuri sana katika ufundishaji wa neno la Mungu ijapo yeye bado suala la kufuata nyayo za familia yao ya kichungaji hataki kulizungumzia kabisa.
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: