Jumapili, 4 Novemba 2012

KANISA NCHINI KENYA LASHAMBULIWA

Polisi nchini Kenya wanasema watu kama 7 wamejeruhiwa kwenye shambulio la guruneti dhidi ya kanisa katika mji wa Garissa.
Polisi ndani ya kanisa liloshambuliwa mwezi Julai mjini Garissa

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya na televisheni ya Kenya, KTN, wanasema idadi ya watu waliojeruhiwa inaweza kuwa kubwa zaidi na baadhi ya majeruhi ni mahatuti.
Afisa mmoja amesema kanisa hilo lilikuwa ndani ya kambi ya polisi na guruneti liling'oa paa wakati wa ibada.

Wengi waliojeruhiwa ni askari polisi.
Mji wa Garissa uko karibu na mpaka wa Somalia.
Mwezi wa Julai watu 15 walikufa katika mashambulio kama hayo dhidi ya makanisa mjini Garissa.
 
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni