Jumatano, 10 Oktoba 2012

PASTOR PETER MITIMINGI AMALIZA SEMINA YA KUSIFU NA KUABUDU KWA KUWAASA WAIMBAJI NA WAPIGA VYOMBO, KITABU NA DVD ZA SOMO HILO ZINAPATIKANA.

 Mchungaji Peter Mitimingi amemaliza semina aliyokuwa akifundisha katika kanisa la TAG Magomeni kwa kuwaasa wapiga vyombo, waimbaji, watunzi pamoja na watumishi wa bwana.
                                              Mch Peter Mitimingi akifundisha Magomeni TAG

Semina hiyo ya siku 4 alifundisha somo kusifu na kuabudu huku akifundisha kiundani somo hilo. alisema kumekuwa na dhana potofu ya kusifu na kuabudu katikati ya kanisa na wengine kudhani kuwa wanaopaswa kuimba ni kwaya na waongoza sifa tu au kusifu na kuabudu ni pale tu tunapokuwa kanisani. akifafanua juu ya dhana hiyo alisema kuwa kila mwenye pumzi anatakiwa kumsifu Mungu na kusifu na kumwabudu Mungu kunafanyika kila wakati uwe nyumbani, kazini au mahali popote ni wakati wa kumwabudu Mungu. tukimwabudu Mungu katka roho na kweli kuna vifungo vingi vinafunguka na mungu huacha kila kitu anachofanya na kusikiliza pale anaposifiwa maana yeye anakaa katika sifa. na ndiyo kitu kikubwa tutakachoenda kufanya kwa Mungu, maombi yanaishia hapahapa Duniani, Kuhubiri, Kutoa nk lakini kusifu na kuabudu ni jambo litakalo dumu milele.

  kuhusu watunzi alisema kama watunzi wa nyimbo za injili wasipojaa neno watatunga mipasho badala ya nyimbo za kumsifu na kumwabudu Mungu na ndiyo maana kuna baadhi ya nyimbo ukisikiliza kuanzia unaanza hadi unaisha hakuna maneno ya Mungu hapo lipo tatizo mtunzi mzuri ni yule anayetunga wimbo kufuatana na neno la Mungu linavyo sema. alizungumzia na wapigaji vyombo kuwa mara nyingi wamekuwa ni watu wenye viburi na wakimaliza kupiga vyombo wanatoka nje na kwenda kupiga story mpaka waitwe tena kuja kupiga vyombo hawabebi Biblia, wawasikilizi mahubiri. wapigaji kama wao hawafai. na upande wa waimbaji nako amesema wako waimbaji ambao wanajiona wao ndo wao na akisarekodi albamu ndo basi saa nyingine wanatoka hata kwenda kufanya huduma bila ya kuaga. wanatakiwa kutulia na kufuata taratibu wa wachungaji wao ili Mungu awainue.
vile vile alifundisha juu ya watumishi wa Mungu ambao kwao kipindi cha kusifu na kuabudu kwao ni mwiko siku zote wanaingia ibadani baada ya kipindi cha sifa sasa wanasifu wapi?. na wakati mwingine utakuta tena anawainua waimbaji kwa kusema hebu leteni pambio moja tuchangamke na wakati huo kanisa lilisha changamka kwani walisha sifu ila yeye tu ndo amepoa kwa sababu hakuwepo wakati wa sifa anatafuta upako wa kuanzia, aliwataka watumishi kuonyesha kwa vitendo kama Biblia inavyoonyesha katika kitabu cha Joshua kuwa waliongoza waimabaji kuzunguka mji wa Yeriko.

semina hiyo ilirekodiwa siku zote 4 na DVD zinapatikana kwa bei rahisi ya sh 7000 tu na vitabu vyake vinapatikana kwa sh 5000, unaweza kupata kwa kupiga no 0655699284 au unaweza kufika VHM makao makuu mwenge mkabala na hospitali ya mama ngoma.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: