Ijumaa, 12 Oktoba 2012

KONGAMANO KUBWA LA KWAYA DAR KUKUTANISHA ZAIDI YA KWAYA 50 NI TAR 13-14/10/2012

Section ya Magomeni na Kinondoni kwa pamoja zimeandaa Kongamano kubwa ambalo litakutanisha kwa zaidi ya 50. kongamano hilo litafanyika katika kanisa la Revival Kinondoni lililoko kitua cha kanisa maeneo ya Biafra. taarifa nilizozipata tamasha hilo litaanza saa 4:00 asubuhi siku ya jumamosi na saa 8:00 mch siku ya Jumapili. katika kongamano hilo kwaya zote zitaimba na kutakuwa na mafundisho ya neno la mungu.

waalimu katika kongamano hilo ni Mch Christopher Mlaponi wa TAG Kinondoni, Mch Mwalubalile wa TAG Hananasifu na Mch Magembe wa TAG Majumba sita. kati ya kwaya hizo zipo kwaya kongwe kama Revival Kinondoni Victory choir nayo ya kinondoni na nyinginezo nyingi. mtu  yeyote hata kama siyo mwana kwaya unaruhusiwa kuhudhulia kongamano hilo

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni