Jumatano, 19 Septemba 2012

WAKRISTO WAKOPTI KUKAMATWA MAREKANI

Maafisa wa utawala mjini Cairo, wameamuru kukamatwa kwa wakristu saba wa kikopti raia wa Misri wanaoIshi nchini Marekani kwa kuhusika na utengezaji wa filamu iliyozua ghadhabu miongoni mwa waislamu wengi kote duniani.
 
Filamu hiyo ambayo inamkejeli mtume Muhammad ilizua ghasia na kero katika mataifa ya kiisilamu kwa namna ilivyomdhihaki Mtume.
 
Hata hivyo haijabainika mtunzi wa filamu hiyo lakini imehusishwa na wakristo wa kikopti wanaoishi nchini Marekani.

Kibali cha kumkamata mchungaji Terry Jones nchini Marekani kimetolewa.

Mwanamke mmoja na wanaume saba akiwemo Jones, wanatuhumiwa kwa kuitusi dini ya kiisilamu na kuchochea ghasia za kidini , kwa mujibu wa taarifa za mwendesha mkuu wa mashtaka.

Taarifa hiyo ilisema kuwa shirika la polisi wa kimataifa la Interpol, watafahamishwa kuhusu vibali hivyo.

Ombi pia litatolewa kwa maafisa wa kisheria nchini Marekani. Inaarifiwa kuwa ikiwa wote waliotuhumiwa watapatikana na hatia huenda wakahukumiwa kifo.
 
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni