Jumatatu, 17 Septemba 2012

UJERUMANI YATAKA KUMPIGA MARUFUKU PASTOR TERRY JONES KUHUBIRI KWAO

Chansela wa Ujerumani, Angela Merkel, amesema kuwa serikali yake itampiga marufuku mhubiri mmoja tatanishi kuingia nchini humo.
 
Kasisi Terry Jones, anayesifika kwa vitisho vyake vya kuiteketeza Quran nchini Marekani, amealikwa kuhubia mikutano kadhaa za mashirika ya watu wenye siasa kali.

Bi Merkel alisema kuwa ikiwa mpango wake utafanikiwa hatapewa visa kuingia nchini humo.
Bwana Jones amesema kuwa anaunga mkono filamu iliyozua kero miongoni mwa waisilamu kote duniani hasa Mashariki ya Kati.

Mwandishi wa BBC mjini Berlin, anasema kuwa makundi yenye siasa kali nchini Ujerumani ambayo yamemwalika, yanataka kuionyesha filamu hiyo hadharani.

http://www.youtube.com/watch?v=6Vr0OKTTkjc
 
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: