Ijumaa, 3 Agosti 2012

MAISHA MAGUMU MUISRAEL MWINGINE AJICHOMA MOTO

Raia wa pili wa Israel amekufa baada ya kujichoma moto akipinga hali ngumu ya uchumi na kukosa usawa.

Akiva Mafi alikufa kwa majeraha ya moto alipojiwasha mwenyewe katika kituo cha basi mwishoni mwa mwezi Julai.
Baadhi ya watu wakiwasha mishumaa kuomboleza

Bw Mafi aliyekuwa akitumia baiskeli ya walemavu ambaye pia ni afisa mwandamizi wa jeshi katika umri wa miaka 40 rafiki zake walisema amekuwa katika mzozo kuhusu mafao yake.
Kitendo chake cha kujichoma moto kimetokea wiki moja baada ya Moshe Silman kujichoma mwenyewe akipinga mkutano wa hadhara Tel Aviv alikufa wiki mbili baadaye.
Siku ya Jumanne serikali ya Israel ilipitisha kifungu kipya cha kubana matumizi na kuongeza kodi kama sehemu ya kupunguza matumizi.
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni