Jumanne, 14 Agosti 2012

KAMA HUKUFIKA JANGWANI BASI PATA HABARI NA PICHA ZA MATUKIO YA LOVE TANZANIA FESTIVAL WALIOMLETA DON MOEN TANZANIA

Love Tanzania festival iliteka jiji la bongo wiki iliyopita kwa mambo mengi katika kueneza habari njema za Yesu kristo. kwa mimi kama mdau wa injili nilijifunza mambo mengi katika kuwakusanya watukuja kusikiliza injili. utakubaliana na mimi kuwa siku za leo mikutano ya injili imepoteza mvuto na watu wengi hawaendi tena kwenye mikutano, kila mmoja ana sababu zake lakini hawa waliweza kukusanya maelfu ya watu katika viwanja ya jangwani kwa siku 2.

walianza kwa kugawa miwani bure, kutembelea shule na vyuo mbalimbali katika kuwashirikisha upendo wa Mungu na kukutana na wanawake na watu wenye taaluma mbalimbali katika viwanja vya Karimjee. huko kote walikuwa wakizungumzia upendowa Mungu na baadae walienesha mafunzo ya mpira wa miguu kwa watoto katika viwanja mbalimbali na walifaya mambo meni sanakwa ajiri ya watoto.

haikuishia hapo Jangwani kulikuwa na michezo mingi ya watoto na wali enjoy sana watoto katika mkutano huu, ukiacha michezo pia alikuwepo mtaalamu wa nyimbo za watoto Duggie Dug Dug.. na kulikuwa na michezo ya baiskeli ambao niliona vijana wanaochezea baiskeli wa pale morocco nao walikuja kuona wanavyofanya wengine, na pia mchezo uliowavutia wengi na kuogofya wengi ni ule wa kuruka juu sana na pikpiki kiasi kwamba kuna baadhi awau waliogopa hata kuangalia mchezo huo amba kwa mara ya kwana umeonyeshwa live hapa TZ. watu wengi walikuwa wanaongoa kuwa walikuwa wanadhani michezo hiyo inanogeshwa na kompyuta kumb ni kweli.

ukiaca hiyo michezo ukija kwenye jukwaa lilikuwa la kisasa sana na blog hii iljuzwa kuwa lililetwa kutoka Uganda ni jukwaa la ubora wa kimatifa na vyombo vya mziki ndo usiseme. waimbaji wote waliimba live kasoro msanja mkandamizaji na hii ilileta radha ya pekee japo kulikuwa na utofauti kati ya waimbaji wetu na wale waliotoka Marekani ambao walionekana wana uwezo mkubwa katika kumiliki jukwaa kupiga vyombo na hata kuimba live kuliko wa hapa kwetu.


the Voice ambaao wao hutumia mtindo wa akapera walionyesha ukongwe wao katika kuzitumia sauti zako na walifanya vizuri sana, wengine ni Upendo Kilahilo ambaye aliitumia sauti yake nzuri kusha mbulia jukwaa na kati ya nyimbo alizoimba ni Zindonga wimbo unaopendwa na wengi, Pastor Safari naye alikuwepo aliimba wimbo wake Hakuna Mungu kama wewe, Christina Shusho aliimba nyimbo nyingi ukiwepo ule wa Nipe macho. kilichonifurahisha ni kule kuimba nyimbo zao live bila chenga na waliweza kuimba nyimbo zaidi ya mbili kila siku.
ukiacha mahubiri ambayo yalihubiriwa na Andrew Palau ambako mamia ya watu waliokoka, waimbaji kutoka Marekani walifanya vizuri kuonyesha ukongwe na uzoefu katika utumiaji wavyombo vya mziki na sauti zao na radha ya muziki waliokuwa wakipiga na kuimba ni kama wameeweka cd vile. Dave Luben ambaye aliimba nyimbo nyingi kwa kiswahili utafikiri naye ni mswahili na waimbaji wote walijitahidi kubadilisha baadhi ya mabeti ya nyimbo zao na kuziimba kwa kiswahili akiwemo Duggie Dug Dug Nicole na Babu Don Moen hiyo ilifurahisha sana na kufanya watu kuzidi kufuatilia kwa umakini kile kilichokuwa kikiendelea pale uwanjani.
waliyewachangamsha sana na kukusanya watu ni babu Don Moen watu wengi sana walifika kumuona yeye maana kwa niaka mingi watu huwa wanaona dvd zake tu lakini wakati huu ilikuwa live bila chenga alipokuwa akikaribishwa kuimba uwanja mzima ulikuwa ukiripuka kwa kelele na vifijo kumkaribisha mkongwe huyo wa nyimbo za kusifu na kuabudu naye bila hiyana alifanya makuu kwa msaada wa Mungu na kutuacha tukibubujikwa na uwepo wa nguvu za Mungu " Utukufu ni kwa Mungu" anayewapa wanadamu vipawa na huduma kubwa zinazokubalika Duniani kote. nakumbuka hata alipokuja Ron Kernoly mwaka juzi haikuwa hivi.

zaidi ya yote utukufu na sifa apewe yeye Mungu aliyewezesha yote kufanyika kwa amani na furaha kama duniani ndo hivi je huko mbinguni itakuwaje kaza mwendo tufike huko na kama bado huaokoka mwite yesu yeye ndiye njia ya kweli na uzima ukimpata yeye basi tuonane kule mbinguni kwenye furaha zote.


kwa picha na habari za kikristo unaweza kutembelea page hii na ku like
http://www.facebook.com/Martmalecelablogspotcom/posts/430517270319842?ref=notif&notif_t=share_comment#!/Martmalecelablogspotcom

Picha zingine bonyeza hapa
 http://www.facebook.com/media/set/?set=a.429384317112919.110967.391224594262225&type=1#!/media/set/?set=a.429384317112919.110967.391224594262225&type=1
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni