Alhamisi, 23 Agosti 2012

DON MOEN BAADA YA KUTOKA TANZANIA KURUDI TENA AFRICA SAFARI HII NI ZAMU YA NIGERIA

Mwimbaji wa nyimbo za gospel Don Moen aliyekuwa Tanzania katika viwanja vya Jangwani week mbili zilzopita anarudi tena Afrika katika nchi ya Nigeria, blog hii imefuatilia ratiba ya muimbaji huyo ambayo kwa mwezi huu imeonekana imebana kwa kuwa na ratiba zisizo na mapumziko, baada ya kutoka Dar alifikia studio kwaajili ya kurekodi albamu ya Chrismass zoezi hilo la kurekodi limeemdelea tena kuanzia Jumatatu na linaisha leo na kesho anatarajiwa kusafiri na kuelekea Nigeria ambako atakuwa Asaba katika eneo la delta yadah, pamoja na kuimba katika tamasha lakini atakuwa ma mazoezi na waimbaji watakao msaidia kuimba huko.

Jnne ataondoka Nigeria asubuhi na kurudi New York ambako jioni yake atakuwepo tena kwenye Tamasha lingine la Worship His Majesty litakalofanyika Waldorf-Astoria Hotel.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni