Jumatatu, 23 Julai 2012

WAZIRI TIBAIJUKA AWAOMBA WAKRISTO KUOMBEA NCHI YA TANZANIA NA VIONGOZI WAKE

WAKRISTO nchini wameombwa kuliombea taifa kwa bidii ili Mungu awaongoze viongozi wa juu kwa hekima waliongoze taifa kwa haki, amani na mafanikio katika mchakato wa Katiba mpya.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka alisema hayo juzi na kuwataka waumini hao pia waliombee Bunge ili lisichakachue sheria na kuingiza mambo binafsi na badala yake watunge sheria zenye kuwasaidia Watanzania wote.

Waziri Tibaijuka

Profesa Tibaijuka alikuwa akizungumza kwa niaba ya serikali katika Kongamano la Roho Mtakatifu linaloendelea kwenye Viwanja vya Jangwani.

Kongamano hilo la Kanisa Katoliki, limeandaliwa na Chama cha Kitume cha Karismatiki Katoliki cha kanisa hilo Jimbo Kuu la Dar es Salaam na juzi ilikuwa siku maalumu ya kuliombea Taifa. Profesa Tibaijuka alisema, “Taifa lolote lisilo na hekima hakuna upendo wala haki, njia pekee ya kutekeleza haki ni kupitia hekima ya Mungu, migomo haina faida vijana lakini pia msiwe kama kondoo bali mhoji mambo kwa hekima.”Akisisitiza kuhusu hilo, Tibaijuka alisema Rais, Waziri Mkuu na Mawaziri bila hekima ya Mungu hawawezi kutekeleza majukumu yao na kusisitiza pia kuwa hata Bunge bila hekima hiyo watachakachua sheria.

Awali, Mratibu wa Karismatiki Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Estelatus Mtema alisema maombi hayo ni mahususi kuombea mambo mbalimbali yanayoendelea katika taifa ikiwemo sensa, katiba mpya, migomo, amani na utulivu.Maombi hayo yaliwashirikisha Wakatoliki na baadhi ya Wabunge akiwemo Mbunge wa Mbinga Mashariki,

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni