Jumamosi, 21 Julai 2012

PAMOJA NA KUANZA MFUNGO KIJANA WA KIISLAMU AFANYA FUJO KWENYE MKUTANO WA INJILI

katika hali isiyokuwa ya kawaida kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja amefanya fujo katika mkutano wa injili ulioandaliwa na section ya magomeni unao fanyika TAG Tandale kwa Mch Mshama. mwandishi wa blog hii alishuhudia fujo hizo zikifanyika. Kijana huyo ambaye ni bodaboda alionekana akipita kwa mwendo wa kasi karibu na jukwaa la mkutano mara kadha na baada mhudumu mmoja wa mkutano kumsimamisha na kumuuliza kulikoni unapita hapa mara nyingi bila kujali watu walioko hapa unaweza sababisha ajali. ndipo huyo kijana wa bodaboda alipolipuka kama kamwagiwa mafuta ya petrol na kuanza kutoa lugha chafu ndipo iliamuliwa kuwa akamatwe awekwe chini ya ulinzi wakati wakitoa taalifa polisi. lakini baada ya muda walimwachia na akaondoka na kwenda kusikojulikana. na mkutano ukaendelea.
Hapa vijana wakiwa wamemshikiria kijana aliyekuwa anafanya fujo kwenye mkutano yuko katikati haonekani pichani unaona kamba ambazo walikuwa wanataka kumfunga ili kumpeleka kwenye kituo cha polisi

mara akaja mara nyingine na pikipiki yake na mara hii akasimamisha pikipiki yake mbele za jukwaa na kuanza kutukana kama alivyofanya awali. ndipo ikatolewa tena amri akamatwe na mkurugenzi wa uinjilisti section ya magomeni Mch Seiko, lakini tena akaachiliwa na ikazuiwa pikipiki yake huku wakisubiliwa polisi wafike ili iwe kama ushahidi, baada ya dakika 15 hivyo likaja kundi la bodaboda kama 5 hivi wakiwa wamepakiana wawili wawili na wote wakaingia na pikipiki zao wakapaki mbele ya jukwa na kuanza kufanya fujo na huku yule jamaa wa kwanza akaanza kutembea uwanja wote na kutafuta watu waliokuwa wamemshika mara ya kwanza na kuanza kuwapiga kwa ngumi, Joakimu ambaye ni mshirika wa TAG Magomeni alipigwa ngumi na kuvimba shavu na kwenda kulipoti polisi ili apate RB. baada ya kufanya fujo hizo wakapanda pikipiki zao na kuondoka. pamoja na vurugu hizo zote zikiendelea Mwinjilisti Sote ambaye ni Mchungaji TAG Kizota ambaye ndiye alikuwa ni mhubiri aliendelea kuhubiri na kusema kuwa yeye anaijua Tandale sana maana nae amekulia na kusoma Tandale hivyo halikumshangaza na kuendelea kuhubiri habari njema za Yesu na kusema wao wameleta habari njema na za amani za Yesu kristo.

mpaka mwandishi wa habari anaondoka sehemu ya tukio polisi walikuwa bado hawajafika na ilitolewa gari kwaajili ya kuwafuata, nae Mchungaji Kiongozi wa TAG Magomeni Duastan Kanemba ambaye alionekana kutokufurahishwa na fujo zilizotokea alikuwa akiongea na kiongozi wa mtaa ili wasaidia namna ya kumpata huyo kijana na kumfikisha kwenye vyombo ya sheria. nilipata kuhojiana na watu kadha wengine wakasema kijana huyo alikuwa akifanya hivyo kuanzia mkutano umeanza kila siku anapitapita, na watu hao wakahoji je ungekuwa ni mhadhala au sughuli yoyote ya kiislamu angefanya hivyo kama asingefanya kwanini afanye hivyo kwenye mkutano wa kilokole na wengine wakasema uislam maana yake ni amani sasa yeye mbona anakuwa mshali?   mpaka tunaingia mitamboni tumeshindwa kupata kauli ya waandaaji wa mkutano na kujua hati yake ijapo habari za chini chini zimesena wanataka kufikisha kijana huyo polisi ili alipe ghalama za wale aliowapiga pamoja na gharama za mkutano.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni