Jumanne, 3 Julai 2012

Papaa Ze Blogger Kucheza Filamu Ya Siku Za Mwisho ---666 (End Time) imetungwa na Mchungaji Kaduma, Dokii nae yumo

Soko la "Christian Movies" ambalo kwa Muda Mrefu limekuwa likishikiliwa na Watu walio nje ya "Ufalme wa Kristo" limeingia katika Ushindani baada ya Wakristo Mbalimbali Kuamua Kuingia katika Soko hilo ili kuweza kufikisha Ujumbe wa Neno la Mungu lakini Pia Kufikisha Ujumbe Sawia.

Emmanuel Myamba almaarufu kama Pastor Myamba amekuwa akicheza vizuri zaidi Christian Movies sababu yeye pia ni mtu ambaye yupo kwenye upande unaofahamu nini maana ya nguvu za Mungu na vile zinavyotenda kazi. Katika Filamu yake iliyokamilika na kuingia kwenye soko muda mrefu nguvu za Mungu zilionekana live pale mapepo yalipolipuka Kikwelii wakati wa Shooting.
Filamu Mpya inayotengenezwa inayokwenda kwa jina la "Siku Za Mwisho" a.k.a "End Time" ipo katika hatua za Kukamilika na Mapema Mwa Mwanzoni mwa Mwezi wa August Filamu hiyo itaachiliwa katika Soko la Tanzania na Nje Ya Tanzania.

Filamu hiyo yenye Kusudi na madhumuni ya Kuwakumbusha Wakristo Safari Ya Mbinguni, lakini Pia Kuhusu Unyakuo na Watu Watakavyoishi mara baada ya Unyakuo Wa Kanisa hapa Duniani. Filamu hiyo iliyoandaliwa na Mch. Joshua Kaduma na kuwa Directed na Mr. Mtitu imekuwa ya aina yake sababu filamu hiyo imekuwa ikigusa hata washiriki pamoja na Wanao shoot na kusema hakika kazi hii haitakuwa Bure.

Weekend hii Blog ilizungumza na Mch. Joshua Kaduma na kutaka Kujua maendeleo ya Ukamilishaji wa Filamu hiyo, Mchungaji alikuwa na haya ya kusema "Filamu hii ilianza kama ni Somo la Siku Za Mwisho nililokuwa nikiandaa KWa ajili ya Kanisa ninalochunga, Wakati nilipokuwa nikiandika Somo, Roho Mtakatifu akaanza Kunipa picha, ya maisha halisi ya Kwetu Tanzania yatakavyokuwa Wakati wa Unyakuo, Niliingia kwenye Maombi Mazito na Kumwomba Mungu aliasaidie Kanisa lake. Nilipomaliza Somo, Mungu akanisemesha kwa habari ya kutengeneza Filamu, Nikachukua Notes za Somo nikaenda nazo kwa Wataalamu wa Script Waliposoma somo, na ile Mifano, Wakasema ni Script tosha inayoweza kutengeneza Movie ya Tofauti hapa Tanzania, ndipo Idea ya Movie ikaja rasmi".

Akiendelea kuongea na Mchungaji Kaduma alisema "Mpaka Sasa Filamu Imekamilika kwa sehemu kubwa zimebaki Sehemu Chache za Shooting, na editing na mwisho kabisa mwanzoni mwa mwezi wa nane itakuwa Sokoni. Sasa tunataka Kanisa Kuhubiri kwa njia nyingine kufikisha injili ya Yesu Kristo katika Kizazi hiki".

Baadhi ya Segment zilizo katika Filamu hiyo ni Kama Zifuatazo.

 Pastor Chris, Christopher Mlaponi wa kanisa la TAG Kinondoni ambaye katika Filamu hiyo amecheza Kama Mchungaji anayefundisha Neno Halisi Pasipo Kuchakachua

 Kushoto ni Amos akiwa na Dokii katika mojawapo ya Scene ya filamu hiyo, ampao katika Filamu Wamecheza kama Familia waliyookoka, lakini siku ambayo Baba Wa Nyumba alipata deal ofisini la EPA kama Mil 300 na siku hiyo hiyo ndo Unyakuo Unatokea Mama anaenda Baba anabaki. Dokii na Amos wameonesha Uchezaji wa Hali ya Juu kabisa.

 Kushoto ni Pastor Joshua Kaduma, Mwenye Kuandika Filamu hiyo, Katikati ni Mtitu Director wa Filamu hiyo hapa wakiwa na Tshirt za Siku Za Mwisho.

 Mlimani TV walikuja Location kwa ajili ya Kuchukua maelezo kwa ajili ya Filamu hiyo, Pastor Joshua akitoa maelezo, huku Pastor Kishimba akiwa anasikiliza Kwa Makini.

 Huyu Jamaa amecheza kama Marehemu aliyekuwa akielekea Kuzikwa wakati mchakato unaendelea Unyakuo ukatokea Jamaa akafufuka. Hapa akiingia kwenye Jeneza.

Jamaa akikaa Sawa Ndani Ya Jeneza

Hapa Watu Wakifungungua Jeneza baada ya kuona ghafla Jeneza Limekuwa Jepesi......This is the Most exciting Scene. Location ilikuwa TAG Kinondoni

                                                 Shooting ndani Ya CCC Upanga
Papaa Ze Blogger anacheza kama Senior Mtume na Nabii (Apostle P) ambaye kwenye Mafundisho yake anaweka mkazo kwenye kupanda mbegu na kuwahimiza Watu kuwa  Yesu harudi leo wala Kesho. Na kulegeza masharti mengi sana ya Wokovu na kusababisha Kanisa lake kuwa na lundo la waumini. Katika Scene hiyo Ze Blogger A.k.a Apostle P ameonesha Kipaji Kingine cha Kucheza Filamu.

                                  Senior Apostle and Prophet Papaa (Apostle P) ndani ya Scene

habari kwa hisani ya blog ya samuel sasali

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni