Jumatano, 4 Julai 2012

NIGERIA ITASAMBALATIKA KAMA KUNDI LA BOKO HARAM HALITA DHIBITIWA- DR. DAVID OYODEPO

 
Mkuu wa chuo kikuu cha Agano, mjini Otta, Ogun, Dr.  David Oyodepo, aliupitia kwa upya mfumo wa ulinzi wanchi hiyo kinyume na wale wanaojiita ‘religious bigots’ wanaoitaka Nigeria iwe nchi ya kiislam kwa kuendelea kushambulia makanisa.
Oyodepo pia alitoa wito kwa serikali kujidhatiti kwa swala la tatizo la usalama, kwa kushindwa kufanya hivyo italetezea mgawanyiko. “Naamini kwamba tulichonacho sasa mikononi mwetu ni agenda ya propaganga za uislamu unaodhaminiwa na madhehebu yao na ndio wanaoletezea vita, na serikali isipo fanya uamuzi wa kuzuia haya, Nigeria halitakuwa taifa tena.”
“Hebu tufikirie: Boko Haram, lina lalamikiwa, na wanadai kuwa wenyewe wanapigana na serikali kwaajili ya haki zao, swali ni kwamba je kanisa ndilo linalo husika na haki zao? Kama mabomu kaskazini mwa Nigeria ni kwaajili ya kuleta umasikini katika nchi, kwanini misikiti inaachwa bila kulipuliwa kwa mabomu?

Aliendelea: “Je vikosi vya usalama vilipo kuwa vikipambana kusini, vimewahi kuwakamata waumini katika misikiti siku ya ijumaa? Kinachoendelea hapa ni unafiki wa kisiasa tu.

“Je hakuna waislamu Magharibi, Kusini na Mashariki mwa Nigeria? Kwanini wao hawawapigi watu wanapokuwa makanisani wakiabudu? Kwanini wasiwarushie wakristo mabomu? Ninaamini kuna baadhi ya watu wahana lengo lolote zaidi ya kutaka kuivunja Nigeria”
Oyodepo alisema kuwa kundi la Boko Haram lina igharimu taifa kwa kiasi kikubwa kiuchumi, opotevu wa fedha, ambapo taarifa ya uwekezaji kidunia iliweka fedha za kinigeria trillion 1.3 katika uwekezaji wa ndani. Alisema isipokuwa ajira ndani ya nchi hakuna, taasisi zilizopo ni chache, na makampuni mengi yamekuwa yakiwekeza nchi za jilani kama Ghana, kwasababu makampuni mengi yanaangalia sehemu yenye amani ili yaweze kuendelea.

Oyodepo aliendelea kwa kutoa baadhi ya mifano ya nchi zenye vita Afrika kama vile Sudan, Rwanda, Somalia, Sierra-Leone, Liberia, Congo, Ethiopia, akitaja sababu na muda wa vita katika nchi hizo na athali zilizotokea pamoja na vifo na majeluhi.

Kwa mifano niliyotoa hapo juu inatosha kuifanya Afrika, na Nigeria kukaa kufikiri, na kugundua kuwa bara letu linatakiwa kujifunza juu ya ukweli kua vita havina faida yoyote. Oyodepo ameelezea kuwa wote wanaochochea mauaji ni wabinafsi, wanajijali wenyewe na wameshindwa kufikiria matokeo ya hayo wanayoyafanya.

“Swali la kujiuliza ni kwamba, lini Afrika itajifunza? Watu wa mali bado wanaendelea kuuwana wenyewe kwa wenyewe mpaka sasa. Si kwamba tunajifunza kupitia kusikia bali tufikirie juu ya kile tulicho kisikia. Ni naamini hili ndili tatizo la Afrika kutokujifunza kutokana nakile tunachokiona, kisikiana hata tulichonauzoefu nacho”

Oyodepu aliendelea kusema: “Changamoto kubwa kwa maendeleo ya Afrika ni uwezo mdogo wa kufikiri wa waafrika. Fahamu za wanigeria zinatakiwa zibadilishike kuwa na mtazamo mpya wakuweza kuileta Nigeria mpya” mpaka tutakapo tatua swala la usalama ndipo tutaweza kutatua swala la uchumi wan chi.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni