Jumanne, 31 Julai 2012

MASANJA MKANDAMIZAJI ATOA KALI RUKSA KU BURN

Mchekeshaji maarufu Tanzania ambaye pia ni muimbaji wa nyimbo za Injili Masanja au kwa jina jingine Mchungaji mtarajiwa, ametoa tahadhari kwa wanaombeza kuigiza wakati yeye Mungu hajamwambia kuacha.
Masanja Mkandamizaji akiwa kwenye madhabahu

Msanii huyo ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akihojiwa na mtangazaji maarufu Millard Ayo kutoka radio moja ya kijamii. Hata hivyo hapo kabla Masanja aliwahi kunukuliwa kwamba ipo siku atakuwa mchungaji pia ataacha uigizaji Mungu atakaposema naye.

Mbali na hayo amewatangazia wanaouza CD feki kwamba “nimemaliza kufanya album yangu ya Gospel najua wako watu mamasta wa kuburn kazi za waimbaji nimewakaribisha waburn hii yangu, yani hamna kesi hashikwi mtu atakaeburn kazi yangu kwa sababu hii ni huduma ukiburn wauzie watu hata mia mia usiziweke ndani”

Kwenye sentensi nyingine Mchekeshaji huyu wa Orijino Komedi ya TBC1 amesema “kuna watu wananiambia Masanja tumeona watu wanauza CD feki nasema kama na wewe unaweza nunua na ukatengeneze zako kwa sababu hii ni huduma nataka watu wapate ujumbe huu wabadilike wamjue Yesu tunaemuhubiri mwanawane”

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni