Jumanne, 24 Julai 2012

EE MUNGU TUREHEMU BABA AMWOA BINTI YAKE KWA LAZIMA . WAMEZAA NAE WATOTO 3, ANAISHI NAE KWA MIAKA 28 SASA

Baba mmoja mwenye umri wa miaka 56 amekamatwa na polisi West Virgina kwa kosa na kuishi na binti yake na kuzaa nae watoto 3.

imegundulika kuwa baba huyo ameishi na binti yake huyo kama mume na mke kwa miaka 28 na amepew ujauzito mara 3.

mwanamke huyo ambaye sasa ana miaka 35 aliwambia wapelelezi wa polisi kuwa baba yake huyo alianza kumfanyia vitendo hivyo alipokuwa na umri wa miaka 7 tu. na alipofika miaka 13 alipata ujauzito na kuzaa mtoto wake wa kwanza alipokuwa na miaka 14 na mtoto wa pili alimza akiwa na miaka 19 na wa tatu akiwa na miaka 20.

watoto wao sasa wa kwanza ana miaka 21 wa pili 16 na wa tatu miaka 15. matukio kama haya kwa sasa yamechukua kasi duniani si hapa Tanzania au nje ya Tanzania licha ya sheria kari zinazotungwa bado hazijamsaidia mwanadamu kujitenga na dhambi. hapo ndipo wapendwa tunatakiwa kutambua kuwa siku zimeisha na tunatakiwa kuhubiri injili kila mahali maana mambo yanayotendea nyakati hizi yanashangaza na kusikitisha sana.


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni