Jumatatu, 2 Julai 2012

ALBAMU YA NITANGARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE KUZINDULIWA KANISA LA MAGOMENI TAGMWNJILISTI Kabula George, anatarajiwa kuzindua DVD yake inayokwenda kwa jina la NITANGARA TU, katika ukumbi wa kisasa wa kanisa la TAG Magomeni lililopo Magomeni mikumi nyuma ya kituo cha daladala zinazoenda Buguruni. akiongea na blog hii alisema maandalizi yanaenda vizuri na kila kitu kimekamilika watu waje wamuunge mkono katika uzinduzi huo wa DVD yake.

waimbaji wengine watakao sindikiza uzinduzi huo ni Bony Mwaitege ambaye atakuja na mtindo mpya wa uchezaji, Sarah Mvungi, Ami Mwakitalu, Rose Nyato, Janeth Mrema, Sifa John, Tufaina Mbaga, kwaya ya Revival na Deo-doxer zote za Tag Magomeni. uzinduzi huo unatarajiwa kuanza saa 7 - 12 jioni watu wote mnakaribishwa.


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni