Ijumaa, 8 Juni 2012

TAMASHA KUBWA LA KUMSIFU NA KUMWABUDU MUNGU NA KUOMBEA TAIFA LETU LA TANZANIA LIWE NA AMANI

Mwalimu na mwimbaji wa nyimbo za injili John Shabani Ambaye pia ni kiongozi wa chama cha muziki wa injili Tanzania ameandaa tamasha kubwa kwaajili ya kumsifu na kumwabudu Mungu. sambamba na uimbaji pia yatafanyika maombi ya kuliombea Taifa la Tanzania yatakayoongozwa na wachungaji na viongozi wa serikali watakao hudhulia kwenye tamasha hilo.Wachungaji mbalimbali watakuwepo wakiongozwa na Dr Getrude Rwakatare, mgeni rasmi kwenye tamasha hilo atakuwa ni Mh Dr Fenella Mukangara ambaye ni waziri wa habari, vijana utamadhuni na michezo, viongozi wengine ni Eng Juliana Palangyo, Mh Dk Mary Mwanjelwa MB na wengine watakao kuwepo ni Mr ruge Mutahaba wa Clouds, Msama ambaye ni meneja wa John Shabani na watu wengine wengi.

Stara Thomas ambaye hapo mwanzo alikuwa mwimbaji wa nyimbo za kidunia sasa ameokoka na ametoa cd yake ya nyimbo za injili naye atakuwepo katika tamasha hilo usikose.


waimbaji ambao watapamba jukwaa kwa uimbaji ni Mh Mbunge Martha Mlata, Mzee makasy, Stella Joel, Cosmas Chidumule, Mch Jangalason, Safi , Belle kombo wa BSS, Faraja Ntaboba, Joseph Nyuki, Chistina Shusho Stara Thomas, na kwa upande wa kwaya ni kwaya ya Revival Magomeni na Joybringers kutoka Mikocheni B.

Dr Getrude Rwakatare naye atakuwepo
vile vile John shababi atazindua DVD yake na Blog yake ya Http://www.johnshabani.blogspot.com
ukumbi utakao tumika ni kanisa la TAG Magomeni lililopo nyuma ya kituo cha Mikumi ukiwa unaelekea Buguruni paa la kijani juu kuanzia saa 8:00 Mchana . kila mtu atakayehudhulia anaombwa kuvaa nguo nyeupe na nyekundu na hakuna kiingilio wooooooote munakaribishwa sanaaaaaaaaaaaaa

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni