Ijumaa, 8 Juni 2012

MAANDAMANO NA VURUGU ZA ZANZIBAR KUHAMIA DAR LEO?!! WAPENDWA TUNATAKIWA KUOMBEA AMANI YA NCHI YETU ISIVURUGWE

Baada ya kuwepo na maandamano na vurugu zilizoambatana na uchomaji wa makanisa huko Zanzibar waislamu wamepanga kuandamana leo jijini Dar. maandamano hayo ambayo yamepangwa kuanzia kwenye misikiti mbalimbali iliyopo jijini Dar, na yataishia  kwenye viwanja vya Kidongo chekundu. madai yanayo wasababisha waandamane hayatofautiani na yale ya Zanzibar ijapo mara nyingi wanatafuta tu sababu ya kuanzia. huku bara wana sema kuwa  hawana imani na baraza la mitihani.  Maada Ya 70% Ya Waislam kufeli somo la Divinity lile la "Islamic Knowledge" Walisema wameonewa, haiwezekani 70% waka feli dini yao. Baada Ya wao kufanya Uchunguzi imebainika kuwa Computer za Necta zilikuwa zinakosea kugawanya marks, badala ya kugawanya kwa 2 (Paper 1 & 2) Computer ikawa inagawanya kwa 3, ndio maana walipata Marks ndogo.

Ndio Maana leo Walipanga kuandamana, wanadai huu mfumo umewekwa na Wakristo, na unafanya hivyo kwa darasa la 7, form 2, from 4 na form 6, ndo maana Waislam wanafeli kumbe Computer zilizowekwa na wakristo zinawapunja Marks. lakini huku wao wakiwa wamepanga kuandamana leo nalo jeshi la polisi kanda maalumu halikukaa kimya limepiga marufuku maandamano yoyote kutokufanyika leo. Mohamed Msangi amesema jeshi hilo halioni sababu ya kufanyika kwa maandamano hayo, na badala yake wamewaomba wahusika kufanya mkutano tu. sababu za kusitisha maandamano hayo inatokana na ugumu kwa jeshi la Polisi kutoa ulinzi kwasababu waumini wantokea katika misikiti mbalimbali hivyo watashindwa kudhibiti.

 kwa upande mwingine nilikuwa nawaomba wapendwa tuingie kwenye maombi ya kuombea amani ya nchi yetu, hatima ya amani ya nchi yetu iko mikononi mwa Mungu. tuzipinge hizo roho za kishetani zinazotenda kazi ndani ya watu. mimi nafahamu ambavyo shetani hapendi kuona wandamu wakiishi kwa amani nia yake ni kutuvuruga tu. na shetani hawezi akaja kama shetani anatumia watu, hivyo tumpinge yeye na kazi zake na ninaamini kuwa inawezekana maana tumepewa mamlaka ya kufunga duniani na mbinguni, tuitumie mamlaka ya jina kuu la Yesu Amen

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni