Jumatano, 20 Juni 2012

MWINJILISTI KABULA GEORGE KUGAWA DVD ZA NITANG'ARA TU


MWNJILISTI Kabula George, anatarajia kugawa DVD za albamu ya Nitang’ara Tu kwa kila mtu atakayeingia kwenye Ukumbi wa kanisa la TAG Magomeni Mikumi Julai 8, mwaka huu wakati wa uzinduzi wake.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, Mwinjilisti Kabula alisema ameamu kuweka utaratibu huo, ili kila mtu atakayeingia ukumbini humo aondoke na DVD kwa kuchangia kiasi cha sh. 5,000.

Mwinjilisti Kabula alisema tayari DVD hizo tayari zinapatikana katika maduka mbalimbali yaliyoteuliwa jijini Dar es Salaam.

DVD hizo pia zinapatikana katika mikoa mbalimbali ukiwemo Mwanza, Arusha, Dodoma na Kahama mjini.

Amewataka mashabiki wake kununua DVD halisi ili wanufaike na ubora wa nyimbo hizo, ambazo zinamafundisho kwa kila anayeziangalia

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Mawazo yako ni muhimu sana tafadhali tumia lugha nzuri na tutairusha na wengine waisome.