http://www.facebook.com/events/298374726898828/
Baada ya kufanya Tamasha la KUCHEKA
TENA la mwisho pale Landmark Hotel,Ubungo mwezi wa tatu na hatimaye Arusha
mwanzoni mwa June hatimaye mkali na muasisi wa christian comedy nchini Tanzania
anatua tena jijini Dar es salaam kwa Tamasha lake la nne toka ameanza mwishoni
mwa mwaka jana pale Ubungo plaza.
Yaani ni kucheka na kucheka na kucheka
tena huku ukimsifu Mungu na kujifunza yapasayo kutenda katika maisha yako ya
utauwa.
Tamasha hili litawasimamisha Up Coming
Comedians wa kutosha katika segment maalum ya OPEN MIC, na wale ambao
wamezoeleka kama Richard Chidundo,Gerald Mrema,pilipili,Josephine na wengine
watakuwa sambamba na waimbaji kama Sarah Shila, Deogratius, Meshack, Gee &
Seth, WordAlive and Dar es salaam Gospel Bands,Golden Eagles and 1st
Q dance groups katika kunogesha na kuhudumu pamoja na Mkali wa jukwaa, mtu aliye
dawa.....The King Of Stand Up Comedy,CHAVALA.
Kwa wale wafuatiliaji wa mambo,
naamini LAUGH AGAIN CONCERT SERIES sio jambo geni masikioni
mwao!!
Huu ni ule mfululizo maalum wa
matamasha ya vichekesho na vipaji halisi vya kikristo hapa nchini ambao
unasimamiwa na MC/Comedian na Muasisi wake nchini CLOWN CHAVALA(The King of
Stand Up Comedy) kupitia Chavala Ideas Platform chini ya udhamini mkubwa wa
Great Potentials Ltd.
TAMASHA HILO LITAANZA SAA TISA JIONI
MPAKA SAA MOJA NA NUSU USIKU(3-7:30PM)
NA KIINGILIO KITAKUWA
5000/=
NA 2000/= TU KWA
WATOTO.
Katika SERIES hii bado tuko
Msimu(SEASON) wa kwanza na hili Tamasha lijalo litakuwa Tamasha la tatu kwa Dar
es salaam na ni Episode II. Kama ilivyotaarifiwa mapema Tamasha hili la jpili
ijayo(24th June 2012) pamoja na mawili yafuatayo kwa hapa Dar(Yaani
Tar 23th Sept na 23/30th Novemba-mkesha wa mwisho) yatafanyika
katika
ukumbi wa CITY CHRISTIAN
CENTRE-UPANGA(Mkabala na Mzumbe Dsm)
TAMASHA HILI LIMEDHAMINIWA NA GREAT
POTENTIALS LTD,CITY CHRISTIAN CENTRE(CCC),TOUCHING
VISION,AUTHOR2READERS,WORDALIVE CHURCH,OLYMPUS COMPUTERS AND CHAVALA IDEAS
PLATFORM.
Akielezea mafanikio yaliyopatikana
Chavala amesema;.....Kwa kweli mafanikio ni makubwa sana mpaka sasa ingawa
mengine hayawezi kuonekana kwa macho ya nyama ila itoshe tu kusema mafanikio ni
makubwa mno;yaani toka kule ambako nilikuwa sitambuliki na watu kwa makusudi
walikuwa hawataki kuona umuhimu wa Comedy katika ulimwengu wa kikristo mpaka
sasa ambako wengi wameanza kuelewa, wamepokea na wamekubali,kibali nilichokipata
Arusha kwa mfano ni kikubwa mno kiasi cha kushangaza; kwa sasa nina vijana wengi
sana ambao wamevutwa na kuona nao wanaweza kumtumikia Mungu kwa vipaji vyao kama
vile Comedy,Dance na Mashairi na mengine mengi ya vipaji halisi, hivyo nina
wanafunzi wakutosha na zaidi washika dau,wachangiaji na wanaounga mkono ni wengi
sana na hata wewe unaesoma hapa unakaribishwa kuwa mmoja
wao.
Nimeongeza marafiki na maadui(ingawa
kwangu ni invalid) na nimekuza network base yangu hapa nchini, kwa msaada wa
media ninaamini nitaweza kuyafikia majiji yote nchini na kutambulisha Christian
Comedy na vipaji halisi isipokuwa Tanga peke yake,ambayo haiko katika ratiba ya
msimu huu w kwanza.
Chavala ametoa ratiba yote ya mwaka
iliyobaki kuwa anatarajia kufanya Matamasha makubwa hayo katika majiji yote ya
Tanzania kabla ya Novemba,mpaka sasa matamasha hayo yameshafanyika Dar es salaam
na Arusha na Mwishoni mwa July Chavala atakuwa Mbeya,mwishoni mwa August itakuwa
Mwanza,September ni Dar tena,October itakuwa Dodoma na Mwisho wa Novemba
nitamalizia kwa mkesha pale CCC-Upanga,huu utakuwa ni mkesha maalum wa kumaliza
msimu wa kwanza na utahusisha wasanii wote na wengine wateule ambao wamepata
nafasi ya kushiriki katika matamasha mbalimbali ya msimu huu wa
kwanza!!
Kwa matamasha yote hayo yaliyo mbele
bado kuna mengi na vingi vinahitajika,kama vile Pesa, Laptops,Kamera,Music
system,Sudio na mengine mengi hivyo ikiwa unaguswa
kuhusika/kuchangia/kudhamini/kushauri chochote katika Tamasha lolote wakati
wowote tafadhali usisite kufanya hivyo, tutashukuru mno ingawa tunashikilia haki
ya kutendea kazi au kutunza ushauri wowote ule ujao toka
nje.
Unaweza kutuandikia kupitia lacs.project@gmail.com
au tupigie kupitia +255-(713/753)-883
797....pia unaweza kuchangia kwa benki za simu(M-pesa na Tigo Pesa) kupitia
no.hizo hizo.
Lakini pia unaweza kutembelea
blogs
1.
www.gospelstandardbase.blogspot.com......hii
ina mafundisho zaidi kuhusu Neno la Mungu toka kwa watumishi wa Mungu
mbalimbali
2.
www.chavalapf.blogspot.com.......hii
inahusika na mawazo mbalimbali ya watu mbali ambayo ni muhimu na
yanajenga!
3.
www.kingchavala.blogspot.com......
Hii ni maalum kwa ajili ya shughuli zote na matukio yote yamuhusuyo Clown
Chavala,The King!
Na unaweza kutembelea page ya
facebook; LAUGH AGAIN CONCERT SERIES
Au page mahususi ya
Chavala...
www.facebook.com/KingChavala au
www.facebook.com/chavalapf na
zaidi wale watumiaji wa Twitter mnaweza kumfuataPresident Chavala
@ClownChavala
ANGALIZO;
Kama ungetamani kuwa mwanachama na
unapenda kupata habari kila mara zikiwepo huhusu mizunguko ya Chavala katika
kampeni hii na kufanyika kwa matukio haya kokote kule nchi usisite kutuandikia
kwa e-mail hiyo hapo juu.
Na kwa wale wasanii wanaochipukia na
wale wanaofahamika huko mikoani tafadhali wasiliana nasi mapema kama ungependa
kushiriki katika mojawapo ya matamasha haya kwa namna yeyote
ile.
SHUKRANI;(Na President
Chavala)
Mwisho napenda kutoa shukrani kwa
mashabiki na wafuasi wangu wote ambao ndio wanafanya jambo hili liiendelee
kukuwa siku hadi siku,tunashukuru kwa wachangiaji wa fedha,mawazo,muda na ujuzi;
ninawashukuru wote wanaotuombea na kututakia mema kila wakati majukumu
haya;Ahsante kwa magazeti,ahsante watumiaji wa Social networks kama
Twitter,facebook na blogs na wanahabari wote zaidi redio,magazeti na christian
blogs,kuanzia wanahabari binafsi mpaka wale wanaofanya kwenye makampuni na
Taasiss binafsi na za serikali ambao mmkekuwa mstari wa mbele katika kupigia
debe jambo hili! Naamini Mungu lazima awalipe katika mambo
yenu!
Natambua mchango wa wasanii wengine
katika sanaa hii, maana peke yangu nisingefika popote pale,ahsanteni Emmanuel
Mgaya(Masanja Mkandamizaji); Evance Bukuku(VuvuZela Comedy Show); pamoja na
vijana wangu kama Richard Chidundo;Mrema Gerald, Senior ABBy na MC Manu/pilipili
toka Dodoma na wengine wengi ambao kimsingi mchango wao
unatambulika!
Naamini kila utakapoona tangazo popote
hautasita kufika na kuwaalika wengine au wenzako...tafadhali anza kutekeleza
hayo na Tamasha hili,ubarikiwe sana!!
Unaweza tembelea facebook group yetu ;
http://www.facebook.com/groups/lacs.project
Unaweza tembelea facebook group yetu ;
http://www.facebook.com/groups/lacs.project
Ahsanteni sana na karibuni sana sana
kucheka tena na tena na tena maana kucheka ni dawa na kunaondoa sumu
mwilini!!
Papaa the Blogger sambamba na christian ...bloggers wote katika watakuwepo kutoa nafasi ya kukupigisha kura live ya Dada yetu Christina Shusho ambaye anatuwakilisha Watanzania katika tuzo ya Uimbaji wa injili Africa!!
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Mawazo yako ni muhimu sana tafadhali tumia lugha nzuri na tutairusha na wengine waisome.