Jumanne, 19 Juni 2012

KIKUNDI CHA BOKO HARAM KINACHOLIPUA MAKANISA NIGERIA WAMESEMA HAWATAACHA KUFANYA HIVYO MPAKA WAKRISTO WOTE WAWE WAISLAM


Kiongozi wa kundi la Boko Haram amekili kikundi chake kuhusika na ulipuaji wa mabomu katika makanisa juzi jumapili na kusababisa vifo vya watu 50 kule Zaria na mji wa Kaduna. kiongozi huyo amesema Wanatakiwa kujua kuwa sasa ni wakati wa kurudi katika mapenzi ya mungu, group hilo limesema, kuanzia sasa na kuendelea ama wafuate dini iliyo safi(uislam) ama hakutakuwa na amani kati yao.

Msemaji wa kundi hilo Abu Qaqa amesema kuwa wao wanafanya hivyo kulipiza kisasi kwa yale wakristo waliyoyafanya huko nyuma ya kuwaua ndugu zao waislam na kubomoa misikiti yao ya Zonkwa, Yelwan,Shendam, Tafawa Balewa. alisema kuwa waligeza misikiti kuwa kama madangulo na bar huku wakristo wakiendelea kuishi vizuri na kulindwa na serikali.

hivyo kikundi hicho kimewataka wakristo wote wabadili dini kuwa waislam ndipo kutakuwa na amani. Abu Qaqa alianza kwa kusema. leo allah muweza ametupa ushindi juu ya makanisa ya Kaduna na Zaria ambayo imesababisha vifo vya wakristo wengi. Taarifa hiyp iliendelea kusema kuwa allah amewaagiza waislamu katika quran sura 9 mstari 29 kuweza kuwa vamia wayahudi na wakristo ambao hawamwamini yeye, na mtumishi wake mtume mohammed. wamesema wataendelea kuwaua watoto na wanawake wa kikristo.

Taarifa alihitimisha kuwa wakazi wa Maiduguri, Jimbo la Borno wanapata  mateso kwa sababu hawakuwa saidia kikundi chao wakati wa vita dhidi yao mwaka 2009, anataka Wakazi wa Kano kuchunguza na kubadili njia zao wafuate wanavyotaka wao.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Mawazo yako ni muhimu sana tafadhali tumia lugha nzuri na tutairusha na wengine waisome.