Jumatano, 13 Juni 2012

MUNGU MKUBWA MCHUNGAJI PETROS FOUROTAN ACHILIWA IRANI

mch Petros Fourotan

Taafira zilizoifikia Blog hii mda mfupi kutoka Irani zinasema mch Petros Fourotan amechiliwa HURU kutoka gerezani kuanzia juzi Tar 10 Juni. mchungaji huyo ambae amekuwa kizuizini kwa zaidi ya mwaka sasa.  alitiwa kizuizini na serikali kwa sababu ya imani yake ya kikristo. tunamshukuru kwa kuitunza afya na maisha yake alipokuwa gerezani hayo ni maneno ya mtoa taarifa,  hata hivyo bado kuna mchungaji  Behnam Irani ambaye bado yuko kwenye gereza la Ghezal Hezar. japokuwa afya yake imedhoofika lakini imani yake ni kubwa kwa Yesu. amekuwa akisumbuliwa na maradhi na tatizo la kutokuona vizuri, na hata hivyo gereza hilo limemzuia asionane na dakitari ili ikiwezekana afe kwa mafadhi, wapendwa tuendelee kumwombea ili Mungu amponye na ikiwezekana nae achiliwe. Nchi ya Irani ni kati ya nchi zenye msimamo mkali wa imani ya kiislamu hivyo wakristo walioko huko wanapata tabu sana, tuendelee kuomba neema ya kristo iendelee kuwazukia na giza nene lililotanda huko Mungu apeleke nuru.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni