Jumatano, 13 Juni 2012

CHRISTINA SHUSHO NI LANGO LA WAIMBAJI WA INJILI KWENYE TUZO ZA KIMATAIFA. WATANZANIA INATAKIWA TUMSUPPORT KWA KUMPIGIA KURA.

Najuwa wengi tunajua maana ya lango ni sehemu ya kuingilia sehemu. kwa mara ya kwanza mwaka huu Tanzania imepata mshiriki wa nyimbo za injili ambaye anashindanishwa kwenye kumtafuta mwimbaji bora wa kike barani Afrika, kwanza namshukuru sana Mungu kwa kuiona Tanzania na nampongeza sana Shusho kwa hatua aliyofikia maana tumeona jinsi Mungu anavyomuinua kila itwapo leo mwaka jana alikuwa kwenye mashindano hayo, lakini Shusho peke yake hawezi tunahitajika watanzania kumsupport na kwa kutambua hilo ndiyo maana waandishi wa blog za kikristo Tanzania tumeamua kuinyanyua mikono ya Shusho juu kama walivyo fanya wana Israel kwa Musa ili afanikiwe, kufanikiwa kwa shusho kutailetea sifa nchi yetu ya Tanzania na itafungua milango kwa vizazi vijavyo.

moja ya mikakati iliyopo imeanzishwa kampeni inayoitwa VIVA SHUSHO, VIVA TANZANIA. Bloggers tuko mbele lakini nyuma yetu uko wewe unayesoma habari hii na tukifanya kwa pamoja naamini inawezekana maana kwa msaada wa mungu tutatenda makuu Zab 108:13a anza wewe kumpigia kura na waambie na rafiki zako wapige kura. naamini kazi yako haitakuwa bure.
Fuata link hii kupiga kura http://africagospelawards.com/nominate.html

na fuata maelekezo kama utakwama tuwasiliane tukusaidie.
hapa chini ni picha za kikao na Shusho kwaajili ya kampeni hii

Christina Shusho Martin na Victor
Mch Mwita alikuwepo kwenye kikao hicho
Hapa kikao kimepamba moto

Samueli Sasali akitoa maelezo yakinifu jinsi mchakato utakavyokuwa
Ratiba za matukio mengine tutakuwa tunajuzana ila kwa ufupi Tar 17 Juni Christina Shusho atakuwa Dar Live na tutakuwepo kumsupport na Tar 22 Juni kutakuwa na Special Event Shusho's Night hakutakuwa na kiingilio ila wote watakaohudhulia watatakiwa kupiga kura siku hiyo itafanyika wapi utajulishwa. mwishi wa kupiga kura ni tar 30 Juni na Tuzo zitatolewa Tar 7 july huko Uk.

VIVA SHUSHO VIVA TANZANIA
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni