Alhamisi, 28 Juni 2012

MAHOJIANO YA ALIYE IGIZA FILAMU YA “THE PASSION OF CHRIST” YALIYOFANYWA NA KITUO CHA TELEVISION YA CBN
SCOTT ROSS: Ulikuwa na miaka mingapi ulipokuwa una igiza filamu?
JIM CAVIEZEL: Inavutia. Siku nilipo kubali jukumu, nilipokea simu kutoka kwa Mel. Akasema, habari, mimi ni Mel.' 'Mel yupi?, Mel Gibson, Tom cruise, hivi ndivyo nilivyo wafahamu. Sikuwafahamu kwakuwa ilikuwa ndo mara ya kwanza kusikia jina la kikundi hicho. Akasema, mimi ni Mel. 'Akaanza kunielezea kuhusu filamu hiyo na majukumu ambayo alitaka niyafanye katika filamu hiyo.
SCOTT ROSS: Ulizungumza nini kuhusu hilo? Na hasa baada ya yeye kulileta kwako?
JIM CAVIEZEL: Siku iliyo fuata, alinambia, 'Nataka uwe makini sana kwa kile ambacho utaenda kukifanya. Hauta kifanya tena.'Alilisema hili mara nyingi kwa uwazi. Nika mwambia, 'Mel, hichi ndicho ninacho amini. Kila mtu ana msalaba anatakiwa aubebe. Inanibidi ni bebe msalaba wangu binafsi. Kama tusipo kubali kubeba misalaba yetu tutaumia. Kwahiyo twende tukafanye kazi hiyo. Na ndipo tulipo anza kuandaa filamu hiyo
SCOTT ROSS: Ulikuwa una umri gani?
JIM CAVIEZEL: Nilikuwa na umri wa miaka 33.
SCOTT ROSS: Awali Ulilichukuliaje swala hili?
JIM CAVIEZEL: Kiukweli nilivuta puumzi, huku nikiwa na hofu. Nilikuwa nalifikiria swala hili kila wakati.
SCOTT ROSS: Situ kwasababu wewe ni msanii, lakini je ulijiandaaje kuigiza kama mwana wa Mungu?
JIM CAVIEZEL: Ni swali zuri. Kuwa nilijiandaaje? Kwa moto. Nyuma kulikuwa na maneno mawili, yenye ‘Moto usiozimika,’ kilichokuwa kigumu ni kwamba kuumia kulikuwa  halisi. Nilikuwa nikianza kuanzia saa 8 usiku mpata saa 10 alfajiri nikiwa mwenyewe mahali pale, ilikuwa ni nafasi mbaya, situ mbaya pia lilikuwa ni nafasi iliyo nifanya niwe na wasiwasi. Sikuweza kukaa hata chini. Kadri siku zilivyokuwa zikienda, niliugua, pia mabega yangu yalikuwa kama yametenganisha, ilinilazimu kufanya maombi. Nilifanya hivyo nikimaanisha kabisa nikiwa kama punguani.
SCOTT ROSS: Unasema uliingia kwenye maombi. Je uliamini ulicho kuwa ukiomba kutokana na nafasi ulioicheza? Wewe ni mwamini?
JIM CAVIEZEL: Vizuri, hapakuwa na swali kama niliamini. Nafikiri watazamaji wako wengi wanelewa kuhusu kile ninacho kisema. Kwa nini kuwekewa masharti mwenyewe kwa mateso isipokuwa wewe kujua kwamba hiyo ni kweli? Ngoja ni kwambie,nilikuwa msalabani. Watu wengi walinitazama, naigiza kama Kristo, lakini mara nyingi nilijihisi kama Shetani. Nilikuwa na matusi yakitaka kunitoka. Ilikuwa ni ya baridi ilikuwa ni kama visu vinaingia ndani yangu. Sijui kama umewahi kushughulikiwa kivile, Siku ile nilijisikia baridi sana sikuweza hata kusema. Kinywa changu kilikuwa kikitetemeka sana. Mikono na miguu yangu iliumia sana. Nilizimia pale msalabani. Kwa nusu ya muda, watu walikuwa wakinitazama huku wakicheka.
SCOTT ROSSS:  Ilikuwa kweli kupita miongoni mwawatu mkiwa na kundi la watu?
JIM CAVIEZEL: Hapana, tulikuwa na watu wanao jua huzuni katika hali ya ubinadamu, tulikuwa na watu wenye majonzi, wenye utofauti, na ni watu ambao walikuwa wameguswa na tukio. Kuangalia vile kiubinadamu nilitamani hata kupasuka, nikasema waambieni hao watu wakae kimya, au waondoke.
SCOTT ROSS: Je haikuwa kinyume sana kwa yale waliyomfanyia, na Yesu kuwasamehe maadui zake?
JIM CAVIEZEL: Unafikiri katika hatua hiyo utafanya nini? mimi ni fundi, mimi ni muigizaji. Kwa kumaanisha niliingia kwenye maombi, hayakutoka kwenye ufahamu wangu, yalitoka kutoka ndani ya moyo wangu.
SCOTT ROSS: Wakati unachapwa viboko na kupigwa makofi ilikuwa ngumu kuangalia kwa sababu ilichukua muda mrefu. mimi nilijaribu kuhesabu mapigo. Nilivyo waangalia watu katika ukumbi wa michezo mbele yangu, nikaona wakigeuza mbali nyuso zao kwa sababu hawakuweza kuendelea kuangalia.
JIM CAVIEZEL: Umesema kitu muhimu sana: Watu waligeuza nyuso zao mbali walipo kuwa wakiangalia. Kile walichokuwa wakikiona ni dhambi zao. Sikutaka kushughulika, mara kwa mara, na dhambi zao wenyewe. Ndio maana ni ngumu sana kuangalia. Lakini filamu hii inakulazimisha wewe mwenyewe kujiona, si vile unavyotaka kujiona mwenyewe, bali kamavile Mungu anavyo kuonano wewe.
SCOTT ROSS: Ni sehemu gani ya filamu hii likuwa na athari kubwa kwako?
JIM CAVIEZEL: Kijana acha niwemkweli kuna vitu ambavyo nilivipitia, ni ngumu hata kuvielezea. Nilihisi kama uwepo mkubwa ulikuja ndani yangu wakati tulipokuwa tunaigiza sinema. Yale maombi niliyokuwa nikiomba, sikutaka watu wanione mimi, nilitaka wao wamuone Yesu. Na kupitia vile wokovu utapatikana.' Hicho ndicho nilihitaji kuliko kitu kingine, kwamba watu kuona matokeo na hatimaye kufanya uamuzi wa kumfuata yeye au la.
SCOTT ROSS: Na huo ndio uchaguzi tu, ama kufanya au la. Waigizaji wengi wamekuwa wakishitushwa na filamu ya mateso ya Yesu (The Passion of The Christ). Lakini wachache tu hutambua umuhimu wa kufanya filamu  hii. Ni pamoja na Jim Caviezel mwenyewe. Caviezel alienda kumsaidia mtayarishaji wa 700 Club huko Scott Ross iliaelewe kwa undani zaidi nini maana ya kucheza filamu ya kusurubiwa kwa Mwokozi.
SCOTT ROSS: Filamu ilikuwaje?
JIM CAVIEZEL: Nakumbuka kipengele kimoja wakati naigiza mateso ya Kristo, “unaweza usijali lakini kwetu sisi ilikuwa ni hatari yamkini hata kuvunjika migongo” “Wakati ule msalaba unayumbayumba, na nilikuwa juu ya jabali yapata futi elfu moja. Kama lile jabali lingeli bomoka ingekuwa ni hatari kwangu. Na Mel hakuwa na lakufanya, tulikuwa ndo tuko katikati ya tukio lililokuwa linachukuliwa mkanda kwa wakati ule, na ghafra ulitokea upepo uliovuma kwa nguvu,na kusababisha mlsalaba kuyumbayumba sana nilipokuwa pale juu, japo msalaba ulikuwa umeshindiliwa vizuri lakini sikujihisi kama ni salama na upepo uliendelea kuvuma, na nilikuwa nikiumia kila upande, mabega yakatenganishika, sijui kama umewahi kupitia hata moja ya hayo.
Lakini nilifikiri tumefanikisha, siku iliyo fuata tuliangalia filamu hiyo na ilionekana nzuri sana, Lakini Mel akasema, “Hatuta itumia hii.” Nikasema “Unamaanisha nini kusema hatuta itumia hii?”. Akasema “Kama watu wataangalia msalabani hawata muona Yesu, watakuwa wakiona tu msalaba unayumbayumba. Sahau hii tunaanza tena” ikatuchukua wiki nyingine tano kwaajili ya kipande hicho cha kusulubiwa peke yake.

SCOTT ROSS: Huzuni kweli.
JIM CAVIEZEL: Hiyo ni kwaajilii ya kipande cha kusulubiwa.
SCOTT ROSS: Katika sehemu ya kwanza ya filamu hii nabii Isaya Alisema kuwa Yesu alipigwa, alichubuliwa na alipondwa kiasi kwamba ilikuwa vigumu kumtambua kama yeye ni mtu.
JIM CAVIEZEL: Hatukuweza kufikia kiwango hicho. Na hatukuenda kwa undani zaidi kwa vile tulivyo soma, tulifanya kwa sehemu tu. Tulitaka angalau watu waweze kumwona kuwa ni mtu. Kwa sababu kuna kitu kuhusu jinsi gani inaweza ikapoteza mvuto kwa watu kuangalia na hatukutaka iwe hivyo.
SCOTT ROSS: Pia sijui kama ilikuwa kweli au la!, ulipokuwa uanaigiza ilikuwa kama unapigwa na umeme vile, hii ilikuwa ni kweli?
JIM CAVIEZEL: Nilikuwa natoa hotuba nikiwa mlimani, nilifikiri ule moto utaniumiza kwa dakika nne kabla haujatokea. Nilifikiri “Ungeweza kuniumiza”. Na wakati ulipotokea niliona manyasi katika aridhi yakinyauka.
Walichoona ni kwamba moto ulikuwa ukija kutoka upande wangu wa kushoto na kulia mwa kichwa changu. Ukaning’alizi mwili wote, na walipoendelea kuchukua video wakasema, “unaonekana katika kamera?” kilichotokea wakati Mel amesema “action” kamera zote zikanielekea na kunimulika na hapo ndipo mianga ilitokea. Na wakati kamera zikinielekea, nilimsikia Mel akipiga mayowe, “Nini kimetokea katika nywele zake?” Nilionekana na fanania na staili ya nywele za Don King.

JIM CAVIEZEL: Baada ya kuumizwa kwa dakika tano hivi, Jon Mikalini, ambaye ni msaidizi alikuja na kuniuliza uko safi? Naye akaumizwa, utofauti ulikuwa kwamba wa waliona tu ile bolt ikishuka na kumpiga Jon; hawakuweza kuona kule nilipokuwa nimesimama. Nilihisi kuumizwa kwa kiasi kikubwa sana katika masikio na macho.

SCOTT ROSS: Ulifanya miujiza pale ulipokuwa umeketi. Unaisifiaje miujiza hiyo?
JIM CAVIEZEL: Yeah. Ni kweli palitokea miujiza mingi sana kuliko ile iliyokuwa tayari kufanyika, pamoja na kuumizwa na ile miale ya mwanga, pia Jon naye alikuwa tayari ameumizwa pamoja na kijana mmoja. Lakini miujiza iliyotendeka ilikuwa mingi kuliko miujiza mingine.
SCOTT ROSS: Ulipokuwa umeketi?
JIM CAVIEZEL: Mmoja wa vijana tuliofanya nao filamu hii alikuwa muislam. Yeye alikuwa miongoni mwa wale askari walionipiga, aliamua kubadili dini na kuwa mkristo, alikuwa ni muislam mwenye uzoefu wakutosha,unajua.
Ujue kilichotokea ni kwamba tulikuwa na wakati wakutosha wakufanya maombi tulipokuwa tukiendelea kuigiza filamu hii, na alikuwa anaomba kweli, na kutuombea tulipokuwa tukiendelea kufanya kazi.
Waigizaji wote walioigiza filamu hii, Baadhi yao hawata amini, lakini nafasi itaendelea kuwepo kwaajili yao.
SCOTT ROSS: Unafikiri kufanya filamu hii itakusaidiaje katika kazi yako?
JIM CAVIEZEL: Hichi ndicho ninachojisikia. Na fikiri ilikuwa sahii mimi kuitwa kuja kufanya filamu hii, nikitazama marafiki zangu wa kimarekani na wengine wote duniani, nawaambia waonyeshe imani zao hadharani pasipo kuwa na aibu yoyote. Na ndicho nilichokifanya mimi katika filamu hii. Sifahamu itakuwaje, lakini sita badili mtazamo nitaendelea kufanya kazi hii, na nibado muigizaji, na nitaendelea kuwa muigizaji, hata kama nitapata kazi nyingine ua la!. Nimemaliza kazi yangu. Sasa nimetambua kuwa nilikuwa sahihi, na ilikuwa nafasi yangu, na ninaweza kufanya filamu nyingine ambazo ninzuri zaidi.
JIM CAVIEZEL: Kupitia hii, watu wanapo kuwa ndani ya kristo nakutoka nje ya kristo, na wasioamini wakiwaona. Wana sababisha watu kumkataa, lakini wapo wengine huishi maisha ya kikristo ya kumaanisha wakijua thamani ya mwili wa kristo. Kwa watu kama hao kwao inakuwa ni zaidi ya kumaanisha. Vijana wengi wa kiyahudi wamekuwa na hofu. Watu wa kiyahudi walinijia na wengine walikuwa wakinitumia barua pepe wakiniambia, ‘Jim,’ umewahi kusoma haya mambo? Yana ogofya. Hatukumuua Kristo, Nikawaambia, ‘Hapana, watu walisimama mbele ya Kristo na pilato wakati wa mashitaka wakisikiliza mashitaka yaliyo tolewa na watu wakitaka Kristo auwawe na sio ninyi, lakini pia dhambi zangu na zetu zilisababisha Kristo afe msalabani, naelezea kitu hiki kwakuwa ni muhimu sana watu waelewe. Napenda wayahudi waangalie filamu hii. Na watu wa imani yangu pia. Napenda wapagani na wasio nadini waangalie filamu hii, filamu hii haipo kwa ajili ya kulaumiana. Wote tunahusika katika kifo cha Kristo.


wakati mwingine tuonane ili usome historia yake kama mzeza filamu na historia ya picha ya The passion of The Christ. Ubarikiwe
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni