Jumatatu, 25 Juni 2012

WAKRITO WA KANO NIGERIA JANA WAMEENDA MAKANISANI KAMA KAWAIDA PAMOJA NA ULIPULIWAJI WA MAKANISA ULIOTOKEA JUMAPILI ZA NYUMA

PAMOJA NA MILIPUKO ILIYOTOKEA JUMAPILI ILIYOPITA HUKO BOKO HARAM, KANO BADO WASHIRIKA WAMEJITOKEZA KWA WINGI KWENDA KUABUDU.

waumini wakiwa kanisani
Pamoja na shirika la habari la Reuters kutangaza kuwa kumekuwa na mahudhulio madogo makanisani kwa kuhofia kulipuliwa na mabomu, katika miji ya Abuja na Kaduna, kulikuwa na ulinzi mkali kuzunguka makanisa na katika mitaa mikubwa huko Kano. Katika makanisa mengi magari hayakuruhusiwa kuingia katika maeneo ya kanisa wakati wa Ibada. Askari na Polisi walionekana katika maeneo ya sabongari na maeneo yenye mkusanyiko wa wakristo wengi. Mshirika Simon Adesete amesema kuwa ulinzi mkali uliowekwa umewafariji wa umini wengi na kuamua kwenda kwenye makanisa. Na katika mitaa shughuli za kila siku zimeendelea kama kawaida bila tatizo lolote huku mamia ya watu wamekuwa wakipita na kukaguliwa kabla ya kuingia katika maeneo ya makanisa. Baadhi ya waliohojiwa wamesema ni bora kufia katika nyumba ya Mungu kuliko kwenye kumbi za starehe au mtaani tu. Amesema Franklin Okoye, raisi wa jumuiya ya makanisa ya Abuja .

WAKRISTO WALIO KASIKAZINI WAFANYA MAOMBI ILI AMANI ILEJEEWakristo wanaoishi kasikazini ya Nigeria wamefanya maombi maalumu jana jumapili kumuomba Mungu kurudisha amani tena. Maombi hayo yamefanywa baada ya makanisa kadhaa kulipuliwa na mabomu jumapili iliyopita Kaduna na Zaria.

Pastor Edward Isah wa kanisa la Covenant amewataka wakristo kukesha, kuomba na sio kuchukua sheria mkononi kwa kulipa kisasi.
Isah amewasisitiza washika kuendelea kuomba amani katika nchi yao na Mungu awafariji na kuwafunika wale walio kumba na misukosuko ya makanisa yao kulipuliwa.

Naye , Bishop Idowu Fearon wa Kaduna Anglican Diocese amewaomba wakristo na waislamu waishi kwa amani na waipe nafasi amani katika maisha yao na waishi kwa upendo kama Mungu alivyoagiza.
Fearon ameliambia NAN kuwa mungu aliwaumba wakristo na waislamu ili waishi pamoja kwa amani pamoja na tofauti ya imani zao hapo Kaduna. Na tunatakiwa kuyakubari mapenzi ya Mungu kutuweka kuishi pamoja hivyo kila mtu aheshimu imani ya mwenzake
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni