Ijumaa, 11 Mei 2012

INAWEZEKANA TANZANIA KUWA NA AMANI BILA KUTUMIA MABAVU

Rais Kikwete
Umoja wa makanisa ya kipendekoste Dar es salaam yamepanga kuonana na Rais wa Jamhuli ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho kikwete siku ya jnne ya tar 12/05/2012 katika ukumbi wa diamond jubilee. tarifa nilizozipata zinasema kuwa kabla ya kukutana na raisi wachungaji wote wa makanisa hayo watakutana jumatatu kuweka mikakati waliyoianzisha katika kuimarisha umoja wao na namna ya kushirikiana kuwaleta watu kwa Yesu katika mkutano mkubwa ambao unatarajiwa kufanyika kuanzia tar 15/06/2012 katika viwanja vya Jangwani. aidha taarifa zaidi zimeseka katika kipindi hichi amani na utulivu wa Tanzaania unaanza kuingia dosali baada ya vyombo ya dola kutumia mabavu zaidi katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku, hivyo wao wameona kuna haja ya kuonana na Rais na kuongea nae kuwa amani bila kushurutishwa inawezekana. Polisi wanaweza kuwa hawana kazi kama talativu zilizopo zikifuatwa. aidha kikao hicho kimetanguliwa na maombi ya mkesha yanayofanyika leo (Ijuma) Ubungo TAG pembeni ya Ubungo Plaza, kumwomba Mungu juu ya Tanzania, na ombi lao kwa Rais wanaomba waruhusiwe kuhubiri injili kwa uhuru zaidi, ili watu wengi waokoke na kuacha uharifu na mambo maovu ambayo yatawapunguzia kazi police na jamii itaweza kuishi kwa amani.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK martmalecela
Chapisha Maoni