Ijumaa, 11 Mei 2012

HISTORIA HUJIRUDIA DR JOHN SAMUEL MALECELA ATUNUKIWA CHEO CHA U CANON KANISANI DODOMA

Baada ya kulitumikia Taifa la Tanzania kwa muda mrefu na kusitaafu Dr John S. Malecela, kanisa la Anglikana Dayosisi ya Kati limemtunuku Tuzo ya Heshima ya u- Canon Waziri Mkuu na makamu wa kwanza wa rais wa zamani, John Malecela kutokana na mchango wake wa kutumikia Taifa kwa uaminifu na kutambua mchango wake katika kanisa ndani ya Dayosisi ya Kati. Akimtunuku tuzo hiyo, Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dodoma, Godfrey Mhogoro alisema Malecela ni mfano wa viongozi bora ambao wametoa mchango katika uongozi wa nchi na kanisa wa ujumla.
Canon Dr John Samuel Malecela
Askofu Mhogoro alisema tuzo hizo hutolewa kwa kutambua kazi mbalimbali za watu walioangaliwa kutokana na ushauri wa kiroho ambapo kanisa linatambua na kuthamini mchango wao. “Mzee wetu John Malecela anatunukiwa tuzo ya Canon kwanza akiwa mwenyeji wa Dodoma ameiwakilisha Tanzania katika utumishi wake akifanya kazi ndani na nje ya nchi kwa uaminifu mkubwa. Pia alitumika kama Makamu wa Kwanza wa Rais, kama kanisa tumeona kazi njema alizofanya na sasa milango iko wazi kwa kutoa mawazo na michango yake katika maendeleo ya kanisa,” alisema Askofu Mhogoro. Pamoja na Malecela, watu wengine 10 waliotunukiwa tuzo hizo ni Finias Ntemo, Ernest Kongola ambaye alikuwa Mkaguzi wa Shule za Kanisa za Anglikana kabla ya kutaifishwa mwaka 1967, Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Kati, Daud Tandila, William Chinameta ambaye ni katekista, John Tandu ambaye ni mlei, Avelina Mnyangolo ambaye ni mlezi wa Mvumi, David Mwendamaka, Mzee Madore, Mzee Brian na Richard Morris. Akihubiri katika Ibada hiyo, Askofu Mhogoro aliwataka watu wote kuwa na upendo wa kweli na kufanya kazi kwa uaminifu mkubwa ili kuhakikisha kuwa maendeleo yanapatikana kwani bila upendo hata amani hutoweka. Ibada hiyo na mkutano wa Sinodi ya 18, ulihudhuriwa na wachungaji na wajumbe 794 wa Jimbo la Dodoma, kitu ambacho Askofu Mhogoro alisema haijawahi kutokea mkutano kuhudhuriwa na waalikwa wengi hivyo.
Canon Malecela akiwa mke wake Anna Malecela Nyumbani kwake seaview
Huko nyuma Mzee Yohana Malecela aliwahi kuwa mishenari na kwa kushirikiana na wamiishenari wa kizungu ndiyo walivyo anzisha makanisa mengi ya anglikani mkoani Dodoma. hivyo kwa kupata cheo hicho cha kanisa anaungana na wajukuu wengine wa mzee Yohana Malecela ambao walikuwa ni wachungaji nao ni Canon Naftali Lusinde na marehemu Canon Stephano malecela na sasa Canon John S. Malecela.
Mmishenari Yohana Malecela Babu yake na Canon John S. Malecela

Hii ndo historia yake... http://www.mwananchi.co.tz/magazines/61-miaka-50-ya-uhuru/16964-john-malecela-tingatinga-msafisha-njia.html nyingine: http://www.facebook.com/pages/John-Malecela/112905752055463
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK martmalecela

Hakuna maoni: