Jumatano, 4 Aprili 2012

MAAJABU YA DUNIA KIJANA AFUNGA NDOA NA MAITI ILI KUTIMIZA AHADI YA UPENDO

Kijana mmoja Chadil Deffy  katika nchi ya  Thailand amefunga ndoa na  girlfriend wake ambaye amekufa ili  kutimiza ahadi yake ya upendo.  Kijana huyo mwenye umri wa miaka 29 na mchumba wake mwenye umri wa miaka 28 anayeitwa Sarinya Kamsook walikuwa wamepanga  kuoana mwaka huu.

Sarinya Kamsook kwa bahati mbaya alifariki katika ajali ya gari, siku moja kabla ya tukio kubwa la harusi yao, Deffy aliamua kuendelea na harusi yao kama ilivyopangwa. Sarinya alihusika katika ajali mbaya ya gari, na kupata majeraha makubwa. Madaktali walijitahidi kumhudumia . Hata hivyo madaktari wakiwa katika jitihada za kuokoa maisha yake ili na kuchelewa kumhamishia hospitali nyingi badala ya ile aliyokuwa amelazwa kuna na msongamano mkubwa. Na alifariki baada ya masaa sita. Ibada hiyo ya harusi iliunganishwa na ibada ya mazishi iliyofanyika katika kitongoji cha Surin, Thailand, kijana Chadil Duffy alimvisha pete mpenzi wake huyo ambaye ni  marehemu. Na tukio hilo likawa ni tukio la kipeke kutokea hapa duniani ambalo ni ibada ya harusi na mazishi kwa wakati mmoja.
"Deffy na Sarinya alikuwa pamoja kwa miaka 10, na hatimaye waliamua kukaa chini. Walikuwa wameahirisha  harusi mara kadhaa, kutokana na kutokupata muda muafaka na ukweli kwamba Deffy alitaka kumaliza elimu yake kabla ya kufunga  ndoa. Hata hivyo, baada ya kifo cha mpenzi wake Sarinya Deffy aliona hakuna kizuizi cha yeye kutimiza shauku yake ya kufunga harusi na mchumba wake huyo, hivyo aliamua kufunya harusi kabla ya kumzika. Sherehe hiyo ya Kibuddhist  ilifanyiaka katika mji wa Surin kaskazini mwa Thailand. Deffy  alisema mbele ya jamaa na marafiki waliokuwepo katika sherehe kuwa  ibada hiyo amefanya ili kuonyesha upendo wake mkubwa  kwa Sarinya. Marafiki na jamaa kadhaa walihudhuria harusi hiyo, na tukio hilo lilivuta hisia za watu wengi nchini humo na kufanya TV ya taifa ya nchi hiyo kurusha tukio hilo live. Hadithi, pamoja na picha kutoka kwenye harusi hiyo sasa vimevuta hisia za watu wengi katika internet, hivyo kuzua mijadala kadhaa. "

Wana mziki wengi nchini na nje ya Thailand wamekuwa wakitunga nyimbo za mapenzi na kuweka picha za harusi hii ya ajabu kutokea hapa duniani.

Picha mbali mbali za Sarinya Kamsook alizopiga miezi michache kabla ya kupatwa na ajari

Wapenzi hawa wawili wakiwa pamoja

hii ilikuwa Januali Sarinya Kamsook akifanya shoping

Wapenzi hawa wawili wakiwa pamoja hii ilikuwa mapema mwishoni mwa mwezi Januari

Picha 4 zinazoonyesha tukio la kufunga harusi, akimvisha pete, akimbusu,
Kama una maoni yeyote niandikie hapo chini
Chapisha Maoni