Jumanne, 3 Aprili 2012

JITIHADA ZA KUOKOA MACHO YA ASKOFU ALIYEMWAGIWA TINDIKALI NA WAISLAMU ZINAENDELEA HUKO ISRAELI.Madaktari wa hospitali ya sheba katika mji wa Tel-Aviv huko Israel wanaendelea na harakati za kuokoa macho ya askofu mmoja kutoka nchi ya Uganda ambaye inasemeka alimwagiwa tindikali na waislam wenye msimamo mkali. Habari zaidi zimesema kuwa jicho lake moja liharibika sana kiasi kwamba halitaona tena na lililobaki lina hatihati ya kuathiriwa na tindikali hiyo. Inasemekana alimwagiwa tindikali hiyo baada ya kuvamia nyumba yake wakati wa usiku. Askofu huyo anayejulikana  kwa jina la Umar mulinde jicho lake moja limepoteza uwezo wa kuona kabisa. Madaktari hao ambao hawajui hadi sasa ni tindikali ya aina gani iliyotumika, na wako kwenye juhudi za kuokoa jicho lake la kushoto ili lisiharibiwe na tindikali hiyo.

 Shirika la habari la compass lilimkariri askofu huyo akisema  kwamba ingawa jicho lake moja limeharibiwa vibaya lakini kwa neema ya Mungu madaktari wanajitahidi kadri ya uwezo wao kusaidia kunusuru jicho lililobaki ili lisiharibike na jopo hilo la madaktari wanafikiria hata kung’oa jcho lake la kulia lililo haribika ili lililo baki lisiathiriwe na tindikali hiyo. Pamoja na hayo askofu huyo amefarijika na kusema ijapo wameamua wao kwa imani yao kutenda hivi lakini huduma yangu inasonga mbele huko Namasumba, rafiki yangu Zachariah Serwadda ambaye aliwahi kutekwa na kuteswa sana anaendelea na kazi vizuri. Waislamu hao ambao wana mtandao mkubwa nchini humo baada ya kufanya unyama kwa askofu Mulinde waliandika walaka na kuutupa chini wakieleza nia yao ya kuendelea kufanya vitendo hivyo kwa watu watakao kuwa wakimhubiri Yesu.

 Wakati huohuo nchini Somalia waislamu wenye msimamo mkali ambao wako kwenye kundi la al-shababu wamemuua kwa kumkata kichwa kijana mmoja anayeitwa zakaria Hussein Omar mwenye umri wa miaka 26 aliyekuwa akifanya kazi kwenye shirika moja la kikristo ambapo pia ofisi zake zilichomwa na moto. Kijana huyo aliyeuwawa mwaka huu mwili wake uliokotwa masaa machache baada ya kuuwawa. Kuuwawa kwake kumetokana nay eye kuamua kumpokea Yesu akiwa katika nchi ya Ethiopia, miaka saba iliyopita yeye na familia yake ambao sasa walikuwa wamehamia hapo.

 Kumekuwa na mambo mengi wanayofanyiwa wakristo katika nchi zenye msimamo mkali wa imani ya kiislam kutokana na wao kufuasha sheria za sharia ambazo ni sheria za kiislamu.  Mapema mwezi wa pili baba mmoja wa kiislamu alijikuta akisurubiwa vilivyo na waumini wenzake baada ya watoto wake wawili kumpokea Yesu na kuamua kuokoka katika mji wa Kismayo. Baba huyo Mo’alim Mohamed alichukuliwa hatua hiyo baada ya kulaumiwa kutowafundisha watoto wake kujifunza imani ya kiilamu Quran, huku wakimwambia kwamba kama angefanya hivyo ni wazi kuwa watoto wake wasingeokoka. Huku akijitetea baba huyo alisema kwamba alifanya sehemu yake kama mzazi ila wao watoto tu ndio waliamua kubadili dini na kukimbia kuhofia kuuwawa katika kijiji chao. Kukimbia kwa watoto hao kumewafanya waislamu hao kumweka baba huyo kizimbani mpaka watoto wake watakaporudi. Jambo ambalo hata kama wakirudi adhabu yao itakuwa ni kifo tu, Na hii si mara ya kwanza kwa wazazi kukamatwa kwa makosa ya watoto wao. Katika mji wa Mogadishu mji mkuu wa Somalia kundi la al- shababu limemuua kijana mwenye umri wa miaka 17 aliyekuwa mlinzi wa chuo cha Biblia kijana huyo ambaye alihamia akitokea nchi ya Kenya alifuatiliwa na alshababu tangu mwaka 2008, wapendwa unapokuwa kwenye maombi endelea kuwakumbuka wakristo walioko kwenye mazingira magumu na hatarishi ili Mungu aendelee kuwatia nguvu katika kazi ya Mungu.

KAMA UNA MAONI YOYOTE AU MCHANGO WA MAWAZO NIANDIKIE HAPO CHINI UBARIKIWE
Chapisha Maoni