Jumanne, 20 Machi 2012

NGUVU INAYOTUMIKA KUOMBA KULA ITUMIKE KATIKA KUTATUA MATATIZO YA WANANCHI WA ARUMERU MASHARIKI

wote tunajua kampeni cha uchaguzi mdogo wa jimbo la Arumeru mashariki zinaendelea kwa mbwembwe na nguvu kubwa kwa kila mgomea kuuza maneno yake kwa wananchi. baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kufariki dunia. mimi ninachojua mwezi huu wote utakuwa na vurugu na pilika pilika nyingi na kila mgombea kupiga mluzi wake. na huku wanchi wakipoteza muda wao mwingi katika kampeni na si kwenye shughuli zao za maendeleo ya kila siku . ukiachilia hilo ni gharama zinazotumika katika uchaguzi na huku baada ya uchaguzi wanawaacha  wananchi na shida zao bila ya msaada wowote na wabunge wengine hukimbilia kukaa mijini! nafikiri kuna haja ya wagombea kuwa na hofu ya Mungu ili wanapochaguliwa kweli warudi kwa wananchi wao na kutimiza ahadi walizotoa.

mara nyingi imetokea waheshimiwa hawa kuonekana wakati wa kampeni tu na baada ya kupata ubunge hawaonekani tena nafikiri iwe vyema watimize ahadi zao tena kwa mbwembwe kama walivyokuja kuomba kura. kuna vitu katika uchaguzi huu kuona haviko sawa baada ya mgombea kunadi sera zake na kueleza atawafanyia nini wananchi utakuta mtu anabaki kusema mtu mwingine. kwa kufanya hivyo inakuwa inajenga chuki na kuwagawa katika makundi bila sababu yeyote. katika jimbo la Arumeru vyama viwili ndio vimeonekana kuwa na nguvu kubwa navyo ni chama tawala cha CCM na chama cha chadema ambao wanaonyesha ushindani mkula. hivi sasa zimebakia wiki 2 ili kufikia uchaguzi pamoja na yote tunatakiwa kujua kuwa baada ya hapo maisha wa arumeru yataendelea na atakaye shinda atakuwa na changamoto ya kutimiza ahadi na kuwaweka wana Arumeru bila kuwabagua kichama. na itakuwa ungwana kabisa kutimiza yote wanayoahidi ili kujenga imani kwa wananchi wao.

kila mtu anajua kinachoendelea huko kuna kauli chafu zinatumika katika kampeni hizo na ahadi teletele zisizotekelezeka kwa wanachi ndizo zinatawala kwa sasa na hii inanikumbusha mwalimu wangu shule ya msingi alinipa tafsili ya siasa kuwa ni uongo uliokomaa sasa kama wote tunajua hawa watu wanatupiga changa la macho inabidi tuwe nao makini. wana Meru chakueni mtu mnayemuona kuwa anfaa kutakua matatizo yenu na si uzuri wa sura au ujengaji wa hoja na msikubari kugombanishwa na vyama ninyi ni ndugu uchaguzi ukiisha utarudi mtaani mwako sasa kama utagombana na jirani yako kwaajili ya uchaguzi utawezaje kuishi nae. fikiri kabla ya kutenda.


Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.

Hakuna maoni: