Jumatano, 21 Machi 2012

KANISA LINATAMBUA WAJIBU WA KUWAFUNDISHA VIJANA (TEENAGERS) JUU YA MAHUSIANO (MAPENZI)


Kwanza nichukue nafasi hii kumshukuru Mungu kwa kunivusha salama bila kuumizwa wakati nikiwa teenagers kutokana na mda mwingi kuwa na mazungumzo na vijana wakike na wakiume kuna jambo ambalo nataka leo tushirikiane je kanisa linatambua wajibu wake katika kuwafundisha vijana wadogo.
Nianze na mfano huu. Kuna mnyama Swala huyu mnyama huwa anazaa mtoto na mtoto huyu baada ya dakika zisizozidi 15 huwa anakuwa na uwezo wa kukimbia kama Swala mkubwa. Ila inategemea kazalia wapi mara nyingi huwa naona hata kwenye TV Swala akizalia katikati ya wanyaka wakali kama Simba Chui nk ujue mtoto huyo atakuwa chakula chao maana wanamfukuza mpaka wamkamate bahati mbaya zaidi hawa wanyama wakali wanakuwa wanajua kuwa aliyezaliwa ni mtoto hivyo humfukuza yeye tu mpaka amkamate. Kwa hiyo kupona kwa Swala mtoto kunategemea atazaliwa wapi. Akizaliwa sehemu ambako hakuna wanyama wakali basi atakuwa nay eye mpaka kuzaa la kazaliwa kwenye wanyama wakali ujue yeye anakuwa chakula cha wanyama hao.

Nimefuatilia katika makanisa yetu huwa hayana mafundisho ya hwa vijana wadogo na sit u kanisa lakini hata wazazi wengi huwa hatujihusishi kabisa kufuatilia hata marafiki wa watoto wetu na kujua kuhusu mahusiano. Inabidi leo nitunie maneno makali ili itusaidie kufahamu tatizo lililoko katika jamii yetu kwa sasa. Watoto wanapo balehe na kuvunja ungo ni wachache huwa wanapata kufundishwa kwa habari za madhala ya kuwa na mahusiano, nahisi labda wakati mwingine huwa tunadhani watoto bado wadogo mmmh. Lakini si watoto wa leo wanahitaji wafundishe ili wajue wao kuchagua kati ya mbivu na mbichi. Na wakati mwingine wazazi tukiwa tumeokoka tunadhani kuwa nao wameokoka na kumbe unakuja kukuta wanapitia changamoto mbalimbali na mihemuko ya kimapenzi na wakati mwingine wanashindwa kujizuia kwa sababu wahajui wafanyeje si vema kuhisi hivyo tuwafunze.
Watoto kama hawa wanatakiwa kupata mafundisho sabiti

                    Ngoja nikupe kisa kimoja ambacho kilimpata mtoto mmoja wa kike yeye alivunja ungo! Kitendo hicho kilimshitua maana hakuwa amewahi kufundishwa chochote juu ya hilo. Na akakosa mtu wa kumuuliza akaenda kuuliza rafiki yake anayeitwa abdallar(si jina halisi) sasa abdalar kwa sababu yeye alikuwa anafahamu mambo hayo alichukuwa nafasi hiyo katika kumtega swala huyu mtoto yeye alimwambia anayodawa na atamfundisha namna ambayo itasababisha asi bleed tena. Dawa aliyompa ni kufanya nae ngono na Yule mtoto kwa kutokujua aliridhika na dawa aliyoshauriwa na Abdallar na kujua kuwa hilo ndiyo mwisho wa tatizo lake. Mwezi uliofuata ikatokea tena akafanya naye ngono mwezi wa tatu akautana nae tena sasa Yule mtoto akawa mkati kwa kuona mbona dawa ya Abdallar haiponyeshi?! Ndipo hapo Abdallar alipomwambia mbona hiyo ni kawaida ya wanawake wote kila mwezi lazima u bleed. Ilimuuma sana Yule mtoto wa kike lakini it is too late, maji yakimwagika hayazoleki bahati mbaya Abdallar alikuwa na AIDS na akawa amemwambukiza binti huyu. Mfano huu unasikitisha sana maana kama wazazi wangechukua nafasi yao vizuri mtoto huyu asingepata madhala yaliyompata. Lakini vilevile tunasahau kuwa mwanadamu yeyote hawezi kujitenga na mapenzi kwasababu yapo ndani yetu hivyo basi tunatakiwa kutoa elimu ili watoto wetu wawe salama. Iko faida sana ya kumfundisha mtoto kwanza unajenga msingi tangu akiwa mdogo vile vile njia hiyo hataiacha mpaka atakapo kuwa mzee siku za leo wazazi tunagungua tabia mbaya za watoto wengi wakiwa wameshafikia wakati wakutokubadilika na baada watoto wawe baraka wana kuwa miiba katika familia zetu pata hadithi nyingine nayo ni ya kweli inasikitisha.

                 kuna hii nayo ilipatikana kanisani, pale mchungajai aliyealikwa kutulisha neno alipoamua kutushirikisha matatizo yanayowapata kondoo wa bwana. kuna  siku alipigiwa simu na wazazi fulani aende nyumbani kwao akamuombee binti yao mdogo mtoto wa darasa la nne, kisa cha kuitwa ni kuwa yule mtoto anasoma hizi shule za academia,siku moja asubuhi wakati anawahi basi la shule alisahau kuzima fan (pangaboi la juu) chumbani kwake, kupitia kioo cha juu ya mlango wazazi wakaona pangaboi linazunguka baba akaamua aingie chumbani kwa binti  akazime ghafla akakutana na vidonge juu ya meza ya kusomea....akamuita mama akamuuliza ni vya nini? lahaula vilikua ni vidonge vya majira ya uzazi, wazazi wakahamaki sana wakajiuliza maswali mengi, wakakubaliana wamsubiri binti akirudi jioni wamuulize.

                        Binti aliporudi akabanwa na wazazi, mwanzo alitaka kugoma, wakamtishatisha akakubali kuwa amepewa na Mlinzi wa getini hapo nyumbani, mazingira wanayoishi ni katika estate ina nyumba kama kumi na tano, so the whole compound imezungushiwa ukuta na ina geti moja kubwa la kuingilia.Mtoto akaanza kueleza kuwa mchezo huo  aliuanza miaka miwili iliyopita na fundi mwashi aliyekuwa anajenga hapo estate ndo alianza kumfundisha Ngono, tena aakafuata Mlinzi, mlinzi aliponogewa akamwambia mwenzie, huyu wa plili akamtishia mtoto kuwa asipompa na yeye atamsemea kwa baba yake, mtoto akampa, akaja wa tatu, huyu ndo akamfundisha na kutumia vidonge, sasa akawa mtaalam.

                  Mchungaji alipoitwa akasema kabla sijamuombea naomba mnipe muda nikae nae mimi na yeye tu nimfanyie counselling, hapo ndipo yalipofumuka mengi makubwa, yule mtoto akakiri mbele ya baba mchungaji kuwa ameshazoea sana mchezo wa ngono hata hapo kwenye estate wanapoishi ameshatembea na wababa wanne, huwa anaaga anaenda saloon weekend akifika nje hao wababa wanampakia kwenye magari yao wanampeleka huko wanapopajua kumfanyia uharibifu, akaendelea kueleza  kuwa hata dereva na konda wa school bus tayari ameshafanya nao, shuleni amefanya na walimu wawili na Mwalimu mkuu pia.

             Mchungaji hakuwaeleza wazazi extent ya uharibifu aliyofanyiwa mtoto wao, aliwaita wote akawaombea, next akaenda kwenye hiyo shule kupambana na mwl mkuu, ushauri wa mwisho aliwapa wazazi ni kumwamisha binti shule, pamoja na kuendelea na maombi kwa binti huyo..........................story hii iliwatoa machozi watu kanisani.

               Mtoto wa darasa la nne wewe unadhani ni mtoto kumbe kasha kuwa na huko njiani anakutana na Simba, Chui wakimuinda na kama hatuta wafundisha watoto wetu usidhani hawatatafuta elimu hii watapata ila watafundishwa kinyume si kwa kufuata neon la Mungu haitoshi kumwambia mtoto usizini anatakiwa ajue kuwa kuna foolish age ambako kunakuwa na mihemuko ambayo mtoto asipokuwa ngangali anazini hivi hivi Kikubwa kinachojitokeaza hapa ni hii style ya maisha ya sasa, wazazi tupo too busy na kazi, kutafuta hela kiasi hatupati kuwa karibu na watoto wetu, sasa upweke wanaoupata watoto ndo wanatumbukia kwenye mambo ya ajabu kama haya. Kuna dada mmoja kazini anajua kama mimi nimeokoka akanitania na kusema sikuhizi hakuna anayeolewa akiwa bikira nikamuuliza zinaenda wapi akaniambia zinatolewa na watu. Mimi iliniuma na ni changamoto kwangu wengi ambao wameokoka sasa hawakukulia katika maisha ya wokovu lakini tumeokoka tukiwa tumeshakuwa watu wazima ni asilimia ndogo ya waliokoka katika familia za walokole na ambao hata hao wengi ukiwauliza watakwambia foolish age iliwabamiza na kuwapeleka puta na kujikuta wanaonja na wengine kunogewa na kupotea mpaka sasa hawapo katika wokovu kuna wapendwa wengi nawafahamu ambao hapo mwazo watoto wao walikuwa walokole wazuri lakini sasa si walokole tena. Kuokoka kwa mzazi si kuokoka kwa mtoto kila nafsi inatakiwa itubu, na yale ambayo tuliyapitia sisi kabla ya kuokoka basi iwe changamoto ya kuwafundisha watoto wetu wasirudie makosa yetu.
Kumomonyoka kwa maadili inatookana na jamii kuruhusu tabia za kigeni kutawala na kutowafundisha watoto wetu

                   Lakini vilevile wachungaji, na viongozi wa makanisani tunatakiwa kufundisha masomo ya mahusiano. tuwafundishe vijana wetu ili wapone kama kanisa halitawafundisha watafundishwa na Dunia na akifundishwa na Dunia usimlaumu Mungu maana muda wa kumkunja samaki angali mbichi utakuwa umepita kitakacho fuatia ni kuvunjika kama utalazimisha kumkuja. Tufuatilie kwa karibu nyenendo za watoto wetu marafiki zao mazingira yao ya shule usiwaamini asilimia 100 uliyeokoka ni wewe na wao tuwape msingi mzuri ili wakuwe na kujua nini maana ya kuokoka na tuwe na urafiki nao tukiweka tabaka inakuwa mbaya na ukiwa mbali nao jua una weka mwanya wao kuwa karibu na mtu mwingine. utashangaa mtoto unampa kila kitu lakini anakonda kupe teyari amekuwa muathilika ana ugonjwa wa kupenda. tunakazana kufundisha neno la Mungu tu. kuna mtu aliniambia kuwa miili haiokoki wakipata nafasi wanaitumia miili ya vizuri katika kutenda dhambi.
Leo nishie hapa lakini bado sijamaliza na nitaendelea na somo hili ili litusaidie tusipojenga msingi mzuri kwa watoto wetu tunasababisha kuleta familia zisizobora hapo baadae inaanza na wewe chukua tahadhali


Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.

Hakuna maoni: