Jumapili, 25 Machi 2012

IRAN YAWEKA MIKAKATI YA KUUFUTA UKRISTO

  Nchi ya Irani imeweka mikakati ya kufuta ukristo nchini humo.habari kutoka Tehearani makao makuu ya Irani hiyo zinasema imeanzisha mpango maalumu wa kumaliza kabisa ukristo katika nchi hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ikiwa Israel itaamua kuishambulia nchi hiyo basi wakristo hao wanaweza kuwa vibaraka wa Israel kwa kuvujisha siri zao. Mwandishi wa habari wa mashirika ya habari ya kimataifa wameripoti kuwa wameshuhudia wakristo wakikamatwa kama kuku na kutupwa gerezani huku wakitafutwa kama wezi mitaani.

Askari maalumu walimkamata mmoja wa wakristo  mashuhuri Bw Majid Enayat kazini kwake Februari mwaka huu na kumchapa na kuweka gerezani. na hiyo si mara ya kwanza kukamatwa mwaka 2009 alipolejea kutoka Uturuki alikamatwa na kutupwa rumande lakini baadae aliachiliwa. inaelezwa kuwa baada ya kumkamata Enayat polisi walimlazimisha na kwenda naye nyumbani kwake na kumsachi na kumnyang'anya nyaraka zake zote pamoja na mkanda wake wa harusi ambao waliutumia kuangalia watu wote waliohudhulia ambao ni marafiki wake wa kikristo na kuwakamata na kuwatesa sana na kuwatupa gerezani na wengine teyari wmesha funguliwa mashitaka ya kuukana uislam ambayo adhabu yake ni kifo. na mke wa Majid ambaye ni mtu aliyemsaidia mumewe kuhudumia wakristo katika ibada za nyumba kwa nyumba alipofikishwa katika geleza la Alef-ta ward kwa uchunguzi alijitahidi kuulizia wafungwa wengine ikiwa mumewe  bado yuko mahali hapo lakini hakupata jibu.

wapendwa inatakiwa tuendele kuwaombea watakatifu walioko katika nchi za kiarabu wanateswa sana na kuuwawa ila tujue damu yao haimwagiki bure ila itasababisha watu wengi waokoke injili ya Yesu ni lazima isonge mbele hakuna mtu awezae kuzuima injili amina.  Sifa za Bwana zivumeeeee, zivume vuuuuuuuuuuuu mpaka maka na madina!!!??? mbarikiwe Bwana Yesu.

Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.
Chapisha Maoni