Jumatano, 1 Februari 2012

Ushuhuda wa matendo makuu ya Mungu

Mr David alishuhudia Mungu alivyomtetea kazini kwake na kupandishwa cheo kuwa mkuu wa kitengo

Mr Mgita na mkewe walishuhudia Mungu alivyoweza kuwaponya kwenye ajari ya gari lao wakati wanatoka Msoma kuja Dar na familia yake gari iliumia sana lakini wao walitoka wakiwa wazima kabisa sifa kwa Bwana.

Mr emanuel Malunda yeye alishudia Mungu alivyomponya mama yao ugonjwa wa ukoma wakati wa maombi ya kumaliza mwaka jana ya siku 3 kavu.

Mr Lumezi Papaa yeye alishuhudia Mungu alivyomsaidia hata kupata ofisi yake mwenyewe maeneo ya upanga huku akiwa hana kitu mungu alimfanikisha na sasa anasonga mbele.

Watumishi wa Bwana wa majeshi katika picha Mch Kanemba na mama Mch

Mtumishi wa Bwana Lutengano katika moja za ibada TAG Magomeni.
Mr&Mrs M'bezi nao walitoa ushuhuda ambavyo Mungu amewawezesha kujenga nyumba yao na kuondokana na mambo ya kupanga.
Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.
Chapisha Maoni