Jumamosi, 10 Desemba 2011

WAPENDWA TUACHE UFISADI WA KIROHO                 Hivi karibuni neno UFISADI limeshika kasi kubwa katika nchi yetu ya Tanzania, hata mtoto mdogo anajua neno fisadi na hata watu hutaniana kwa kutumia neon hilo Fisadi. Mfano fisadi wee, gari lako la kifisadi nk. Nimejaribu kupata maana rahisi ya ufisadi kama linayotumiwa na wengi hapa kwenu nikaona kuwa lina maana ya mtu kujirimbikizia mali nyingi ambazo alitakiwa ale na wenzake badala ya kugawana na wenzake anakula peke yake. Kwa kifupi ndiyo hiyo maana ya fisadi kwa mtazamo wa wengi na si kama kamusi .

Nchi yetu imeingia kwenye tatizo hili la usisadi na baadhi ya viongozi wenye nafasi na mianya ya kupata pesa wamefanya hivyo kwa maslahi yao na kuacha wananchi wengi wakiwa hohehahe. Lakini mimi nimeona kuwa hata wapendwa tu mafisadi tena wakubwa tumekuwa mapepali, wabinafsi, na kumfanya Yesu ni wawalokole tu na si vinginevyo. Tena tumezifungia nguvu nzake ndani yetu bila kuzitumia!


TUMEKUWA MAFISADI KIVIPI?

                 Sisi ni tumejaa vipawa na karama ambazo Bwana yesu ametujaza na tumepewa agizo la kutangaza habari za ufalme wa Mungu kwa watu wote haijarishi ni kabila gani ni mweusi au weupe mmasai au mang’ati lakini agizo hili linafanyiwa kazi na watu wachache wengi wetu ni watu wa kukaa makanisani na kuendelea kuliswa na watumishi wa Bwana na kuja na kuja vipawa na karama za rohoni na tunajirimbikizia bila kuwajali wale ambao ni wahitaji ambao tunakutana nao njiani, kazini, mitaani kwetu. Huu nafikiri ni ufisadi mkubwa na mbaya na kwasababu ufisadi ni dhambi hapa sijui kama tutapona, maana Biblia inasema tuwahubiri ulimwengu wote nasi hatufanyi. Na kuna wapendwa wengine wanapiga makelele kuwa kuna mafisadi, mafisadi tena wanasema sanaaaaaaaaaaaaaa na kukasilika kumbe ufisadi mbaya kuliko wote ni huu tulio nao wapendwa.

                Changamoto tuliyona tumwombee Mungu atusaidie ili tuwe na ujasiri wa kufanya kazi yake kwa bidii na bila aibu au kujali mazingila, maana wakati wowote tunatakiwa tuwaambie watu habari za Yesu, na tuwagawie na wengine vitu vya rohoni ambavyo tumevipata kwa Yesu ukiwepo upendo, uponyaji, utajiri wa mambo ya rohoni, amani, furaha na vitu vingine vingi tu. vile tunavyovipata tutamani na wengine wapate na wawe navyo tele maana kama ukiwashuhudia na kuokoka ujue hao ndio watasababisha wewe upate taji. sasa unataka taji? kazi ni kwako chao.


Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.
Chapisha Maoni